POLISI DAR YAWAKAMATA WATUHUMIWA SUGU 586
Jeshi
la Polisi Kanda Maalum Dar Es salaam limefanya msako mkali kuanzia tarehe
22.11.2016 hadi 02.12.2016 na kufanikiwa
kuwakamata jumla ya watuhumiwa sugu 586 wa makosa mbalimbali. Watuhumiwa hao
wamekamatwa maeneo mbalimbali kwa nyakati tofauti tofauti. Wamekamatwa kwa
makosa ya unyang’anyi wa kutumia nguvu,kuvunja nyumba usiku na kuiba, wizi
kutoka maungoni, kucheza kamari, kubughudhi abiria, wizi wa magari, wizi kutoka
maungoni, shambulio la aibu na la kawaida, kutengeneza,kuuza na kunywa pombe
haramu ya Gongo, uvutaji bhangi nk
Operesheni iliyofanyika Buguruni na Magomeni jumla ya watuhumiwa 257 walikamatwa
kwa makosa mbalimbali na jumla ya lita
405 za Pombe haramu za Gongo
zilikamatwa, Mitambo miwili ya kutengenezea gongo na bhangi. Aidha baadhi ya watuhumiwa hao walikutwa silaha
ndongo ndogo za kufanyia uhalifu kama: Visu, nyembe, bisibisi nk. Baadhi ya
watuhumiwa majina yao ni: (1) MARIA NGUTU (81) kabila Mzanaki mkazi wa Kiwalani
alikutwa na gongo lita 200, (2) BENSON
RICHARD(43) kabila Mjita alikutwa na lita 50 za Gongo mkazi wa Kiwalani, nk.
KUKAMATWA KWA GARI AINA YA TOYOTA HIACE IKIWA
IMEBEBA MALI YA MBALIMBALI ZA WIZI
Jeshi
la Polisi Kanda Maalum Dar Es salaam kupitia kikosi kazi chake cha kupambana na
ujambazi wa kutumia silaha, mnamo Tarehe 29/11/206 majira ya saa nne na nusu
huko Kijichi Neluka Mbagala wezi 03 wakiwa na gari no T.129 DDS Noah rangi ya
fedha walivamia baa moja inayofahamika kwa jina la Whatsapp na kuvunja kisha kuiba vitu mbalimbali kama ifuatavyo;
TV flat screen 01 aina ya Samsung, king’amuzi
cha startimes kimoja, Radio 01, spika 02 aina ya sony, na Glass katoni 03.
Askari
wa kikosi maalum wakiwa doria maeneo ya jirani na tukio, walisikia milio ya
risasi na kuwahi eneo la husika kwa
haraka.
Walipokaribia
eneo la tukio walifanikiwa kuiona gari hiyo ikiwa inakimbia kwa kasi. Askari
walifyatua risasi hewani huku wakiwataka watuhumiwa hao wasimame, lakini
majambazi hao hawakusimama na kuendelea
kukimbia.
Ndipo walikosa mwelekeo na kugonga mti na gari
hiyo kusimama hapo hapo na wao wakatokomea gizani kwa miguu.
Askari
walifika kwenye Gari hiyo na kuipekua
vilipatikana vitu vyote vilivyoibiwa kwenye baa hilo.
Jitihada
za kuwakamata watuhumiwa hao unaendelea
POLISI KANDA MAALUM DSM WAKUSANYA TSH 878,670,000/=
KUPITIA TOZO ZA MAKOSA YA USALAMA BARABARANI
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dsm kupitia kikosi
chake cha usalama barabarani kimekamata makosa mbalimbali ya usalama barabarani
kwa kipindi cha siku nne kuanzia tarehe
21/11/2016 hadi tarehe 02/12/2016 na kuingizia serikali mapato ya ndani kama
ifuatavyo;
1.
Idadi ya
magari yaliyokamatwa - 9,817
2.
Idadi ya
Pikipiki zilizokamatwa - 708
3.
Daladala
zilizokamatwa - 3,268
4.
Magari
mengine (binafsi na malori) - 6,548
5.
Bodaboda
waliofikishwa Mahakamani
kwa makosa ya kutovaa helmet na
kupakia mishkaki -
6.
Jumla ya
Makosa yaliyokamatwa - 29,289
Jumla ya Fedha za Tozo zilizopatikana TSH 878,670,OOO/=
Aidha
ukaguzi wa magari na utoaji wa stika unaendelea katika vituo vya Polisi kikosi
cha usalama barabarani na wananchi wapeleke magari yakakaguliwe katika vituo
hivyo.
S.N.SIRRO - CP
KAMISHNA WA POLISI KANDA
MAALUM
DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment