Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Vijana wa Tanzania wenye umri wa chini ya miaka 15, imemaliza ziara Morogoro kwa mafanikio baada ya jana Alhamsi Desemba 8, kuifunga Moro Kids mabao 3-1 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Kwa siku ya jana Ijumaa Desemba 9, mwaka huu timu hiyo ilijifua kwa mazoezi kwa mujibu wa programu ya Kocha Oscar Mirambo baada ya Morogoro kuleta timu ya wakubwa tofauti na vijana wenye umri wa chini ya miaka 15. Hivyo, mchezo huo wa pili haukufanyika.
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini
Kiungo Alphonce Mabula (kushoto), akichuana na Jonathan Kombo wakati mazoezi yaliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. (Picha na Alfred Lucas wa TFF) |
Mazoezi na michezo hiyo ya kirafiki ambayo mingine wataifanya Zanzibar juma lijalo, ni maandalizi ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Burundi mchezo unaotarajiwa kufanyika Desemba 18, mwaka huu kwenye Azam ulioko Chamazi, Dar es Salaam. Awali ilipangwa icheze na Shelisheli ambayo imetoa taarifa ya kuwa haijajiandaa.
Mara baada ya Morogoro, timu hiyo imerejea Dar es Salaam leo kujiandaa na safari ya kwenda Zanzibar Desemba 11 ambako itakuwa na michezo miwili mingine ya kirafiki.
Zanzibar itacheza na Kombaini ya timu ya Vijana wa Zanzibar Desemba 12, 2016 kabla ya kurudiana Desemba 14, mwaka huu na timu hiyo na Kombaini kabla ya kurejea Bara Desemba 15, kujiandaa na mchezo kirafiki wa kimataifa dhidi ya Shelisheli.
Kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu wa timu ya vijana weeny umri wa chini ya miaka 14, Oscar Mirambo anayepata ushauri kutoka kwa Mshauri Mkuu wa Maendeleo ya Soka la Vijana, Kim Poulsen kinaundwa na makipa ni Shaban Hassan Kimwaga na Abdulatif Noor Lema.
Walinzi ni Kareem Bakari Mfaume, Asante Hamis Bwatam, Rashid Hamisi Rashid, Moris Michael Njako, Harubu Juma Tanu, Cosmas Lucas Jakomanya, Salim Abubakar Lupepo na Dastan Daniel Matheo.
Viungo ni Edson Jeremiah Mshirakandi, Jonathan Raphael Kombo, Alphonce Mabula Msanga, Erick Boniface Bunyaga, Gssper Godfrey Gombanila, Sabri Dahari Kondo na washambuliaji ni Jafari Juma Rashid, Ludaki Juma Chasambi, Steven Emmanuel Sodike, Michael Mussa Mpubusa na Edmund Geofray John.
Timu hii inaandaliwa kuja kwa time mpya ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ambao watashiriki fainali za Kombe la Mataifa Afrika kwa vijana mwaka 2019 ambako Tanzania imeteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuwa mwenyeji. Kambi itavunjwa Desemba 18, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment