Monday, January 23, 2017

ACT WAZALENDO WATAJA SABABU ZA ZITTO KABWE KUANDAMWA NA POLISI HADI KUKAMATA GARI LA CHAMA


Juu ya Suala la Polisi Kahama Kuvamia Mkutano wa Kufunga Kampeni na Kuzuia Gari 


Ndugu Watanzania

Magazeti kadhaa ya leo yameandika juu ya Taarifa za Kiongozi wa Chama chetu, ndugu Zitto kutafutwa na Jeshi la Polisi huko Kahama kwa sababu ya Uchochezi kutokana na hotuba mbalimbali alizozitoa wakati wa mikutano ya Kampeni Wilayani humo, hasa zilizohusu tishio la baa la njaa nchini.

Jeshi la Polisi leo limejitokeza kutoa taarifa ya kujikanganya juu ya suala hili hasa baada ya kuhojiwa na wanahabari juu ya sababu za kuendelea kulishikilia moja ya gari lililokuwa likitumiwa na ndugu Zitto pamoja na msafara wake kwenye kampeni za chama huko Kahama.


Kauli ya Jeshi la Polisi ni kuwa walilikamata gari husika kwa sababu walipata taarifa kuwa halina vibali mbalimbali, jambo ambalo si kweli kwa kuwa gari husika Lina vibali vyote vya kisheria. Muda huu Jeshi la Polisi Kahama limeachia gari husika, baada ya kulishikilia kinyume na Sheria kwa siku mbili.

Chama chetu kinalichukulia suala hili la kuwaandama na kuwavizia Viongozi wetu kuwa ni shambulio kwa Chama na Demokrasia yetu, hatutakubali jambo la namna hiyo. Kama Jeshi la Polisi linamhitaji Kiongozi yoyote wa Chama chetu basi lifuate utaratibu na sio kuvamia mikutano.

Msafiri Mtemelwa
Naibu Katibu Mkuu Bara
Kahama
Januari 23, 2017

No comments: