Safari ya Dodoma Gari la Jeshi likiwa limebeba vifaa vya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ikiwa ni safari ya kuhamia Dodoma |
SERIKALI KUHAMIA DODOMA
WAZIRI - OFISI YA RAIS,MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA, MHE. ANGELLAH KAIRUKI AFANYA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU OFISI YAKE KUHAMIA DODOMA*
#Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora leo imeanza safari ya kuhamisha kundi la kwanza la watumishi wake kuelekekea Makao Makuu ya Nchi Dodoma.
#Kundi la kwanza limehusisha Uongozi wa Juu wa Wizara,Maafisa Waandamizi na baadhi ya watumishi wengine - Mhe. Angellah Kairuki.
#Jumla ya watumishi 87 watahamia Dodoma katika awamu ya kwanza - Mhe. Angellah Kairuki.
#Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora itafungua rasmi ofisi yake mjini Dodoma tarehe 30 Januari 2017 - Mhe. Angellah Kairuki.
#Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora itakuwa katika jengo la College of Humanities and Social Sciences lililopo (UDOM) kama makao yake ya muda- Mhe. Angellah Kairuki.
#Anuani ya Posta itakuwa;Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Sanduku la Barua 670, Dodoma- Mhe. Angellah Kairuki.
*IMEANDALIWA NA IDARA YA HABARI (MAELEZO)*
No comments:
Post a Comment