Monday, January 23, 2017

ASKOFU DK. MALASUSA AZINDUA TAWI LA MAENDELEO BANK KARIAKOO

 Askofu wa Dayosisis ya Mashariki na Pwani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa akiweka fedha mara baada ya kuzindua tawi jipya la benki ya Maendeleo la Kariakoo, jijini Dar es Salam, nyuma yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Ibrahim Mwangalaba akifuatiwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Amulike Ngeliama (kulia).  
Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Banki Ibrahim Mwangalaba akiteta jambo na baadhi ya wateja wa kwanza waliyohudhuria ufunguzi wa tawi jipya la Kariakoo. 

Askofu wa Dayosisis ya Mashariki na Pwani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa  akiweka wakfu na kuzindua tawi jipya la Maendeleo banki, Kariakoo wakati wa hafla hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi, Amulike Ngeliama, na kushoto ni Mkuu wa Jimbo la Kati Mch. Frank KImambo

Mkurugenzi mtendaji wa Maendeleo Bank, Ibrahim Mwangalaba akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa tawi la Kariakoo

No comments: