Afisa Mawasiliano ya Umma wa benki ya KCB Margaret Makere akiongea na wanawake wajasiriamali waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali yaliyotolewa na benki hiyo mkoani Arusha.
Katika swala zima la kumkomboa mwanamke mjasajiriamali, Benki ya KCB Tanzania inaendelea na programu ya mafunzo kwa ajili ya wanawake wajasiriamali yanayoitwa 2JIAJIRI. Programu hii inalenga kumkomboa mwanamke mjasiriamali kutoka katika changamoto zinazosababisha biashara yake ishindwe kuendelea.
Benki ya KCB imepanga kufundisha wanawake wajasiriamali 315 kutoka mikoa ya Dar Es salaam, Mwanza, Morogoro, Arusha, Moshi na Zanzibar ambapo matawi ya benki hiyo yapo.
Mafunzo haya ni bure kabisa, benki ya KCB inagharimia gharama zote. na yanahusisha Elimu ya Fedha (Financial Literacy), Kufikiwa huduma za kifedha (Financial Inclusion), Masuala ya Kisheria (Legal Framework), Ushindani wa Kibiashara (Business Competitiveness) na kuwa na sifa za kukopesheka (How to be bankable).
Zaidi ya mafunzo hayo, benki ya KCB itawapatia wanawake wajasiriamali hao maafisa watakao wafundisha kwa vitendo kwenye maeneo ya biashara zao. Maafisa hao watakua ni afisa fedha, afisa sharia na afisa masoko.
Kwako mwanamke mjasiliamali “JIULIZE KWANINI uhangaike wakati benki ya KCB tupo!”
|
No comments:
Post a Comment