Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2016 ambapo umefaulu wa jumla umeongezeka kwa 2.56% kutoka 67.53% mwaka 2015 hadi 70.09% mwaka 2016.
Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Dkt Charles Msonde amesema kati ya wanafunzi 408,372 waliofanya mtihani, jumla ya wanafunzi 277,283 wamefaulu, wakiwemo wasichana 135,859 sawa na asilimia 67.06 na wavulana 141,424 sawa na asilimia 73.26.
Kwa upande wa watahiniwa wa shule, Dkt Msonde amesema kuwa 244,762 sawa na asilimia 70.35 ya waliofanya matihani wamefaulu ikilinganishwa na wanafunzi 240,996 sawa na asilimia 67.91 waliofaulu mwaka 2015.
Kwa upande wa ubora wa ufaulu, amesema watahiniwa wa shule wenye ufaulu mzuri wa Daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60
Shule 10 bora kitaifa
Shule kumi (10) za mwisho kitaifa-Dar es salaam yaongoza
==>Bofya <<HAPA> Kuyaona matokeo ya mtihani wa maarifa (QT) 2016
Bofya HAPA kuona Matokeo Yote
Tovuti ya Necta imeelemewa Kidogo. Tumia Hii Link hapa chini kuyatazama Matokeo
No comments:
Post a Comment