Saturday, February 25, 2017

KIPYENGA CHA UCHAGUZI DRFA CHAPULIZWA,MCHAKATO KUANZA RASMI KESHO


Kamati ya uchaguzi ya chama cha soka mkoa wa Dar es salaam DRFA,imetangaza kuanza kwa mchakato wa uchaguzi wa kuwapata viongozi wa chama hicho watakaokiongoza kwa kipindi kingine cha uongozi.

Mwenyekiti wa kamati hiyo Yusuph Kaiwanga,amesema mchakato huo wa uchaguzi ulipangwa kuanza tangu jana tarehe 24 mwezi februari lakini kutokana na pilika pilika za mchezo wa Simba na Yanga wameamua kusogeza mbele kwa siku moja hadi kesho tarehe 25 mwezi februari.

Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo ni kwamba maandalizi yote kuelekea uchaguzi huyo yamekamilika na ndiyo maana wameamua kupuliza kipyenga na kuwataka wale wote wenye sifa zinazohitajika kujitokeza kuchukua fomu.

Ratiba nzima ya zoezi hilo itabandikwa katika ubao wa ofisi za DRFA,na fomu zitaanza kuchukuliwa kesho hadi tarehe 03 mwezi machi ambapo zoezi la kupitia majina ya walioomba.
Imetolewa na kitengo cha habari na wasiliano DRFA.

No comments: