Meneja mauzo (T-shirt nyekundu katikati) Steven Chen
Kampuni ya simu za mkononi ya itel, leo imetoa msaada wa
vifaa vya masomo kwa wanafunzi wa shule ya msingi Uhuru iliyopo jijini Arusha.
Akikabidhi msaada huo,
afisa mauzo wa itel kanda ya kaskazini Bwana Steven Chen amesema kampuni
hiyo imeona ni jambo jema kusaidia wanafunzi wanaotoka familia zenye kipato cha
chini kutokana na ukweli kuwa wapo wanafunzi wenye uwezo mkubwa darasani lakini
kikwazo chao huwa ni umaskini.Kitu ambacho husababisha kukosa baadhi ya
mahitaji muhimu kwaajili ya masomo kama vile daftari na vifaa vingine kwaajili
ya kujifunzia.
“Sisi itel tunatamani kuwasaidia wanafunzi wote ambao
familia zao hazina uwezo kiuchumi na wana malengo ya kufika mbali kielimu na
kwa bahati mbaya wengine wanaishi na ulemavu.
Tunawaalika pia wateja wetuna wadau wote kwa ujumla kuweza
kutoa misaada yao ili kuhakikisha watoto kama hawa wanaishi kwa furaha na
kutimiza ndoto zao.” Alisema bwana Chen.
Chen aliongeza kuwa, sisi itel tunaamini tukiongeza jitihada
zetu tunaweza kusaidia watoto wengi zaidi na kuwapa upendo na furaha na kujenga
Dunia hii kuwa mahali salama penye upendo na amani. Kwa Pamoja Tunaweza!”
Katika utoaji wa msaada huo, vifaa mbalimbali viligawiwa
kwa wanafunzi takribani 45 ambavyo ni
pamoja na mabegi ya shule, kalamu, penseli,madaftari, rula, mikebe na vingine.
Kwa upande wa uongozi wa shule ya Msingi Uhuru wameishukuru
kampuni ya simu ya itel kwa msaada wa vifaa hivyo kwa wanafunzi. Akitoa
shukrani kwa niaba ya uongozi wa shule hiyo, Mwalimu mkuu wa shule ya msingi
Uhuru, Bi. Rajabu ameziomba kampuni
nyingine kuiga mfano wa kampuni ya itel, kwani kusaidia watoto wa namna hii
kutafanya Tanzania kufuta ujinga na kufanya kuwa Taifa la watu wasomi.
Kwa upande wao wanafunzi wameishukuru kampuni ya itel kwa
msaada wa vifaa vya kujifunzia kutokana na wao kuwa na uhitaji mkubwa.
Akitoa shukrani kwa niaba ya wanafunzi wenzie, amesema wanashukuru
kwa vifaa walivyopatiwa na kuongeza kuwa hii isiwe mwisho kwani wanaendelea
kuhitaji zaidi.
Insert picture.
KUHUSU KAMPUNI YA itel
itel Mobile ni kampuni ya simu ambayo mpaka sasa ina umri wa miaka 10, ni
kampuni ya masuala ya teknolojia na uvumbuzi, iliyojikita kwenye masuala ya
SIMU. Karibu kipindi cha muongo mmoja kampuni hii imekuwa ikitamba kwa
kusambaza bidhaa zake kwenye zaidi ya nchi 45 Duniani kote.
Mwaka 2016, itel iliuza zaidi ya bidhaa zake milioni 50 barani Afrika na
kuongoza kwa kushika nafasi ya kwanza kwenye tatu bora ya Kampuni za simu zenye
idadi kubwa ya mauzo ya bidhaa zake.
Kila unaponunua simu ya itel, unapewa miezi 12 ya kuhudumiwa bure pale simu
yako inapopata hitilafu yoyote ya kiufundi, hii ni kutokana na kuwa na vituo vya
huduma kwa wateja wake baada ya mauzo yaani CarlCare service centers vilivyoko
nchini.
|
No comments:
Post a Comment