Mgeni rasmi wa kufunga mafunzo ya ukakamavu kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza wa Shule ya Jitegemee Sekondari Mgulani JKT, Meja Haule (katikati), akiwa na viongozi wengine wakati wa hafla ya kufunga mafunzo hayo Dar es Salaam leo asubuhi. Kutoka kulia ni Ofisa Tawala wa Kombania wa shule hiyo, Kepteni Zaujia Shemahonga, Msanifu wa Shule, Meja Rehema Wanjara, , Makamu Mkuu wa Shule Utawala, Kepteni Benitho Lubila na Makamu Mkuu wa Shule Taaluma, Ema Mosha.
Paredi la ukakamavu na uzalendo likifanyika.
Gwaride likitoa heshima mbele ya mgeni rasmi.
Ndugu, wazazi na jamaa wa wanafunzi hao wakifuatilia kwa karibu shughuli hiyo.
wanafunzi wa shule hiyo wakifuatilia gwaride hilo.
Gwaride likiendelea.
wazazi wakiwa kwenye hafla hiyo.
Wimbo maalumu ukiimbwa.
Kiongozi wa gwaride hilo, Pelegia Nyunga akikabidhiwa zawadi na mgeni rasmi.
Francis Christopher akipewa zawadi.
Mwanahawa Shabani akikabidhiwa zawadi.
Salehe Hemedi akipata zawadi yake.
Nuhu Sajilo akipata zawadi.
Furaha na utamu wa gwaride hilo.
James David akikabidhiwa zawadi.
Miriam Simon akipata zawadi
Ofisa Tawala wa Kombania wa shule hiyo, Kepteni Zaujia Shemahonga akizungumza katika hafla hiyo.
Makamu Mkuu wa Shule Utawala, Kepteni Benitho Lubila, akitoa hutuba fupi kaba ya kumkaribisha mgeni rasmi.
Wimbo wa taifa ukiimbwa. |
Wimbo wa Taifa ukiimbwa.
Brass Band ya JKT ikiongoza gwaride hilo.
Na Dotto Mwaibale
WANAFUNZI nchini wametakiwa kuacha kujiingiza katika makundi yasiofaa ili kujiepusha na kujihusisha na dawa la kulevya.
Mwito huo umetolewa na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Mgulani, Meja Haule wakati akifunga mafunzo ya ukakamavu kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee Dar es Salaam leo.
"Wanafunzi acheni kujihusisha na makundi yasiofaa ili kujiepusha kuingia katika vishawishi vya matumizi ya dawa za kulevya" alisema Meja Haule.
Aliwataka wanafunzi hao kutumia muda wao wote kwa kusoma ili kutimiza ndoto za maisha yao kwa kupata elimu bora.
Meja Haule aliwataka wanafunzi wa kike kujiepusha na tamaa mbalimbali kwani wao wapo katika hatari ya kupata vishawishi na aliwataka kujifunza kwa wanawake waliofanikiwa na kufanya vizuri kwa kuwa viongozi katika taifa.
Haule aliziomba shule zilizopo chini ya jeshi kuiga mfano wa shule ya Jitegemee ya kutoa mafunzo hayo ya ukakamavu kwani yanawafanya wanafunzi hao kuwa wazalendo wa nchi yao.
Makamu Mkuu wa Shule Utawala Kepteni Benitho Lubida alisema wanafunzi waliopata mafunzo hayo ni 604 na walitumia wiki tatu kufuzu.
Alisema mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo wanafunzi hao wa kujitegemea, kuwafanya wawe na nidhamu, kujiamini, kuwa wavumilivu na kujiamini.
Aliwaomba wazazi wa wanafunzi hao kuwa wa kwanza kutoa mafunzo mbalimbali kwa watoto wao ili kuwajenga katika misingi mizuri kuanzia ngazi ya familia.
No comments:
Post a Comment