Friday, February 24, 2017

KAMPUNI YA RESOLUTION INSURANCE IMEWADHAMINI KAWE JOGGING CLUB KUSHIRIKI MASHINDANO YA KILI MARATHON 2017

Diwani wa Kawe, Mheshimiwa Muta Rwakatare akiongea na waandishi wa habari (hawamo pichani) wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa walivyodhamini Kampuni ya Resolution Insurance kwa Kawe Jogging Club. Mheshimiwa Diwani alitoa shukrani kwa kampuni hiyo

Katibu Mkuu wa Kawe Jogging Club, Al Haj Seif Muhere (wa kwanza kushoto) akitoa shukrani kwa Kampuni ya Resolution Insurance kwa niaba ya klabu yake. 

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Resolution Insurance, Maryanne Mugo (wa kwanza kushoto),  Ofisa masoko wa kampuni ya Resolution Insurance, Laura Lyabandi (wanne kushoto), Meneja mauzo wa kampuni ya Resolution Insurance Nilufar Manalla (watano kushoto), Meneja wa wakala wa kampuni ya Resolution Insurance (njuma)   wakiwa kwenye picha ya pamoja na Diwani wa Kawe mheshimiwa Muta Rwakatare (wapili kushoto) na baadhi ya washiriki kutoka Kawe Jogging Club watakao shiriki kwenye mashindano ya Kili Marathon.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Resolution Insurance Maryanne Mugo (kushoto), akikabidhi tishirt ya jersi kwa Katibu Mkuu wa Kawe Jogging Club Bw. Al Haj Seif Muhere, ikiwa ni moja ya vivaa vilivyotolewa na kampuni hyo kwa ajili ya kuwawezesha klabu hiyo kuweza kushiriki mashindano ya Kili Marathon. Pamoja nao kwenye picha ni Diwani wa Kawe Mheshimiwa Muta Rwakatare (wapili kushoto) na Mwenyekiti wa Kawe Jogging club Bw. Abdul Risasi.

Kampuni ya Resolution Insurance imekabidhi rasmi mchango wao kwa Kawe Jogging Club kuweza kushiriki mashindano ya Kili Marathon yatakayo fanyika Tarehe 26 Februari 2017. Mchango huu ulikua ni mwitiko kwa ombi la klabu hiyo kuweza kushiriki mashindano ya Kili Marathon.

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Resolution Insurance, Bi. Maryanne Mugo alisema kuwa mchango huo upo ndani ya vipaumbele vya kampuni katika uwekezaji jamii hasa katika sekta ya afya.


Resolution Insurance inadhamini uwajibikaji kwa jamii ambayo kwa kiwango kikubwa inalengo maeneo ya vipaumbele vya Elimu, Afya, Mazingira, Ujasiriamali na malengo yake hasa ni kujikita katika masuala ya ubinadamu.” Bi. Maryanne alisema na kubainisha kwamba hii ni mara ya pili wanaidhamini Kawe Jogging Club kushiriki mashindano hayo na inawahimiza wananchi kwa ujumala kujihusisha na mazoezi kwa ajili ya kuwa na afya njema.

No comments: