Mkuu wa wilaya ya Tarime Glorious Bernad Luoga akizungumza wakati wa Hafla hiyo ya maadhimisho ya siku ya kupinga Ukeketaji nchini shughuli iliyokwenda sambamba na makabidhiano ya vifaa maalumvya ukusanyaji wa Takwimu za ukatili kwa jeshi la polisi Vifaa ambavyo vimetolewa na Jukwaa la Mtoto Tanzania CDF kwa msaada wa UNFPA. Akizungumza wakati wa makabishiano hayo Mkuu huyo wa wilaya ya tarime ambapo ndipo mradi wa vifaa hivyo unaanzia kufanya kazi amesema kuwa Wilaya ya tarime pamoja na kuonekana kuwa ukeketaji umepungua kulingana na Takwimu za Hivi karibuni lakini bado Changamoto hiyo ipo kwa kasi katika maeneo kadhaa Huku akizitaja baadhi ya sababu kubwa zinazofanya vitendo hivyo kuendelea. Baadhi ya sababu hiyo ni pamoja na Umaskini ambao umepelekea Tendo la ukeketaji kuwa kama chanzo cha mapato kwa wale ambao wanatekeleza tendo hilo yani mangariba,ambapo amesema kuwa baadhi ya maeneo wamekuwa wakikeketa hadi kufikia elfu ishirini kwa mtu mmoja ambayo ni pesa nyingi kwa Mtu wa kijijini na endapo atapata watu wengi wa kukeketa wanaitumia kama njia yao ya kujiingizia kipato. Ameongeza kuwa pia ipo changamoto ambayo viongozi wa maeneo hayo wanaotaka kuingilia kati mila hiyo wanayokutana nayo ikiwa ni pamoja na Kutishiwa kuuawa na wengine kupigwa na wanavijiji ambao wanaamini katika tendo hilo jambo ambalo amesema kuwa limekuwa likiwapa changamoto kubwa askari lakini pia viongozi wanaotaka kuondoa hiyo mila katika maeneo hayo. Aidha amesema kuwa Vitendo vya ukatili katika wilaya ya Tarime vimepungua kwa kiasi japo kuwa eneo hilo limeendelea kuonekanan kama eneo hatarishi kwa kuwa wafanyaji ukatili wa maeneo hayo wamekuwa wakifanya kweli na kwa kasi kubwa kulinganisha na Mikoa mingime. Pamoja na Hayo Mkuu huyo wa wilaya amewashukuru shirika la CDF kwa kuwekeza katika maeneo hayo kutaka kupambana na ukatili kwani ni jambo la kuigwa kwa mashirika mengine yenye nia ya kufuta ukatili nchini kuwekeza katika meneo ambayo yana ukatili uliokithiri |
Mkuu wa kitengo cha Dawati la Jinsia nchini Tanzania Afande DCP Maria Nzuki akitoa shukrani zake kwa Mashirika ya CDF na UNFPA waliofanikisha kupatikana kwa vifaa hivyo. |
Kamishna wa Polisi Jamii Tanzania CP Mussa .A.Mussa ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika hafla hiyo akizungumza |
Mwakilishi kutoka UNFPA ambao ndio wanunuzu wa Vifaa hivyo Bi Christine Kwayu akizungumza wakati wa hafla hiyo |
Picha ya Pamoja baada ya shughuli hiyo. |
No comments:
Post a Comment