Kampuni ya simu yenye asili ya China, Tecno Mobile
imekuja na ufumbuzi wa tatzo la simu janja (smart phone) kutokaa na chaji kwa
muda mrefu.
Tecno wanajulikana kwa kua na simu zinazokaa na
chaji kwa muda mrefu lakini zikiwa na ubora mkubwa, inatazamiwa hivi karibuni
Tecno wataingiza sokoni simu itakayokua
mkombozi wa watanzania, simu hii inatoka
kwenye mfululizo wa matoleo ya L, ikitanguliwa na L8/l8 plus hii inakuja ni L9
plus .
Tecno L9 plus inatarajiwa na kua betri lenye uwezo mkubwa
Zaidi simu zilizoko sokoni za aina yake,
ikiwa ni 5000 mAh, kwa ukubwa wa betri hili pamoja na matumizi makubwa
kusikiliza au kuangalia video, kupiga picha na kutumia mitandao ya kijamii simu hii inaweza kufika masaa 72 ambayo ni sawa
siku tatu ndipo mtumiaji anaweza kuchaji tena.
Pia Tecno L9 plus pamoja na kua betri kubwa inakuja ikiwa na
uwezo mkubwa kuchaji haraka, mtumiaji akichaji kwa muda wa dakika tano anaweza
kuitumia simu kwa kupiga picha Zaidi ya 1000.
Kwa watanzania walioko mikoani simu hii inawafaa
Zaidi hasa ukizingatia matatizo ya umeme kukatika katika kwa muda usio julikana,
pia kupunguza kadhia ya kutembea na
vibeba umeme, power bank.
Tecno L9 plus inayotarajiwa kuingia sokoni hivi karibuni pia
ina usalama wa alama ya vidole maarufu kama finger print hali kadhalika wemba
wemba mzuri utakao mpa mtumiaji urahisi wa kuitumia.
Inatabiriwa kufanya vizur sokoni na wataalamu wa vifaa
vya mawasiliano, Tecno L9 plus inasubiriwa kwa hamu na watanzania wengi.
No comments:
Post a Comment