Sunday, March 5, 2017

KONGAMANO LA WANAWAKE LA ACT WAZALENDO LAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM


 Chama cha ACT wazalendo kupitia ngome ya wanawake act wazalendo wamefanya kongamano kubwa la kitaifa lililofanyika Jijini Dar es salaam ikiwa ni moja na shughuli ya kuadhimisha siku ya wanawake Duniani.

Kongamano hilo lililohuduriwa na mgeni rasmi Esta Joel Kyamba ambae ni katibu ngome ya wanwake ACT Wazalendo liliweza kuwakutanisha wanawake toka sehemu mbalimbali lengo likiwa ni kujiandaa kuadhimisha cku ya wanawake duniani ambayo kilele chake kitafikiwa tarehe 8 ya mwezi huu wa tatu.
PICHA NA VICENT MACHA

Kongamano limewaweka pamoja wadau mbalimbali toka sehemu mbalimbali kama mwakilishi wa NSSF na daktari wa magonjwa ya kansa wanawake wajasilia mali pamoja wanawake wenye ulemavu kuweza kuwatia moyo na kuweza kuongea nao kuhusiana na changamoto wanazokutana nazo na jinsi wanavyoweza kuzikabiri.

Bi. Stela Kabemela yeye ni muwakilishi wa NSSF alitoa elimu kuhusu umuhimu wa kutumia huduma za NSSF na faida zake.Aliwezakuwashauri wanawake kujiunga na mfuko huo kwa sababu unaweza kuwasaidia kwa gharama za matibabu lakini pia ile hela inakuwepo kwenye mfuko na baadae inarudi kwao tena.

Akiongea na habari 24 alisema pindi mwanachama akijifungua anapewa fedha kama pongezi na wanachama wa kawaida wanaweza kulipa hadi shilingi elfu 20 kwa mwezi.


Mwingine aliyepata nafasi ya kutoa mada katika kongamano hilo ni  DR. Maria Johnson ambeye nae pia alitoa elimu kuhusu kansa kwa wanawake ikiwa ya maziwa na kizazi na alihainisha baadhi ya sababu zinazosemekana ni visababishi vya magonjwa hayo. Aliweza kuwaelezea na dalili za awali za kansa lakini pia wanawake waliofika mahali hapo waliweza kupimwa bure na kuelekezwa jinsi ya kujipima hata wenyewe majumbani na ikiwezekana kuwasaidia wanawake wengine ambao hawakuweza kufika ukumbini hapo kwa maana kansa ni ugonjwa hatari na ni vyema kuuwahi mapema kabla aujeleta madhara makubwa ikiwemo kifo.


Aidha  wanawake waliofika kufika mahali hapo waliweza kufundishwa elimu ya ujasiria mali na jinsi ya kuendesha biashara zao. Dada Aneth Gerema yeye ni mjasilia mali na kiziwi na ameweza kusoma mpaka elimu ya juu ambayo ni degree na baada ya kujaribu kutafuta kazi sana akakosa aliamua kukusanya wenzake na wakaenda sido wakafundishwa jinsi ya kutengeneza bidhaa za viwandani na mpaka sasa kikundi chao kinatengeneza bidhaa mbalimbali ikiwemo Wine, Siagi za karanga pilipili za kopo na bidhaa nyingine nyingi na kwenye siku hii aliweza kuwafundisha wageni waalikwa jinsi ya kutengeneza siagi za karanga.

Baada ya maMbo yote hayo waliweza kutoa zawadi ya mashine ya kufyatulia tofali kwa vijana ikiwa ni kusubirI maadhimisho ambayo wao kama ngome ya wanawake wa ACT wazalendo wataifanyia mvomelo morogoro tarene 8 mwezi huu.







No comments: