Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Sophia Simba ametangaza kutogombea tena nafasi hiyo kwenye uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wanawake wa umoja huo wakati wa maadhimisho ya wiki ya wanawake Duniani yaliyofanyika jijini Dar es salaam.
“Mimi Sophia Simba, nimeamua kutogombea kwa hiari yangu mwenyewe nimeamua kutogombea nafasi ya Mwenyekiti wa Wanawake Taifa UWT katika uchaguzi ujao,”amesema Sophia Simba.
Sophia Simba ametaja sababu zilizomfanya asigombee kuwa ni azma yake ya kuutumikia umoja huo kwa muda wa vipindi viwili tu na si zaidi ya hapo.
Aidha, amesema kuwa akiwa ndani ya UWT amebahatika kushika nafasi mbalimbali za uongozi kwa sababu alianzia nafasi ya ukatibu wa tawi la Kaskazini NDC.
Hata hivyo amesema kuwa anamshukuru mungu kwa kumjalia kushika nafasi mbalimbali kwa kuwa amekuwa mbunge kwa muda wa miaka 22
PICHA NA VICENT MACHA
PICHA NA VICENT MACHA
No comments:
Post a Comment