Ikiwa sakata la Kupotea
kwa aliyekuwa Msaidizi wa Menyekiti wa Chadema Freman Mbowe,Ben Saanane
linaendelea kugubikwa na Utata mubwa huku kila Mtanzania akitamani Kusikia
kijana Huyo alipo hatimaye sakata hilo limetua Meza ya Umoja wa Mataifa ili
kuwapa nafasi na wao kufanya Uchunguzi wake ili kubaini ukweli.
Leo Jijini Dar es Salaam
umoja wa kizazi cha kuhoji Tanzania UTG wamezungumza na wanahabari kuhusu
kupotea kwa aliyekuwa Kiongozi mwenzao katika Umoja huo ambapo yapata miezi
mitano sasa hajulikani alipo huku kila Mtanzania akiwa na hofu kubwa.
Mwenyekiti wa Umoja huo
Malisa Godlisen amewaeleza wanahabari kuwa wamekuwa wakifanya Juhudi kubwa za
kumtafuta mwezao Bila mafanikio ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na Jeshi la
polisi kila wakati japo ameeleza kuwa wamekuwa hawapati ushirikiano mzuri unaoonyesha
matumaini ya kupatikana kwa Ndugu yao Jambo linalowapa Hofu kama wanaweza
kumpata Ben Saanane akiwa salama.
Malisa amesema baada ya
Jitihada zao nyingi wameamua kuwasiliana na vyombo vingine vya haki Tanzania
ikiwa ni pamoja na Tume ya haki za binadamu na utawala bora ambapo
wamewaaandikia Barua ya kuomba wafanye uchuguzi wa wananchi wanaotekwa na
wengine kukutwa wameuawa mitaani pamoja na swala la kupotea kwa kiongozi Huyo
wa Chadema Ben Saanane.
Kuhusu Kituo cha Sheria
na Haki za Binadamu nchini Kinachoongozwa na Bi Hellen Kijo Bisimba, Malisa
amesema kuwa wamefanya mazungumzo na Mkurugenzi wa kituo hicho na kukubaliana
kuwaandikia malalamiko yao Umoja wa mataifa kuonyesha Ushahidi wa Kupotea kwa
utata kiongozi huyo na kama wataridhika watakuja kufanya uchunguzi wao.
“Mama Helen Kijo
Bisimba Juzi alihudhuria mkutano wa umoja wa mataifa ambapo aliibua Hoja ya
wananchi Tanzania wanaopotea kiutata na wengine kuuawa na alijenga Hoja yake
kwa Mfano wa Ben na umoja wa mataifa walishutushwa sana na Hali hiyo kwani
hawakutaraji yanaweza Kutokea Tanzania,Hivyo kupitia kwa kitengo chao cha
uchunguzi wa ukiukwaji wa haki cha OBSERVER wanajipanga kuanza kufanya uchunguzi
wao”.ameeleza Malisa.
Malisa amesema kuwa Hadi
leo Tayari wameshaandika na kutuma Barua ya malalamiko yao Umoja wa Mataifa na
wanasubiri majibu ili kama wataridhika na ushahidi wao waje nchini kuchunguza
sakata Hilo.
No comments:
Post a Comment