Magari ya Zimamoto na Uokoaji yakiwa nje ya Duka kubwa la GSM Mall tayari kuzima moto uliokuwa unaunguza duka hilo katika Barabara ya Nyerere eneo la Mtava, Dar es Salaam. Chanzo cha moto huo hakikuweza kujulikana mara moja.
Mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo akiwahishwa hospitali.
Pilikapilika katika lango kuu la kuingilia duka hilo
Mmoja wa majeruhi akitolewa kwenda kwenye gari ili awahishwe hospitali kwa matibabu
Wananchi wakishuhudia ajali hiyo ya moto
Na Richard Mwaikenda
DUKA kubwa la GSM Mall ililopo Barabara ya Nyerere eneo la Mtava, Dar es Salaam, linateketea kwa moto hivi sasa.
Kwa mujibu wa mashuhuda ni kwamba duka hilo lilianza kuungua majira ya 8;30,Hadi sasa chanzo cha moto huo hakijaweza julikana.
Magari ya zimamoto na uokoaji yamejazana eneo hilo kunusuru mali na maisha ya watu waliokuwemo kwenye jengo hilo lenye ghorofa nne.
Watu wengi wakiwemo wafanyakazi wa duka hilo walionekana kutoka mkuku kuokoa maisha yao. Baadhi yao walitolewa wakiwa mahututi na kukimbizwa hospitali kwa kutumia magari ya polisi.
Duka hilo kubwa la kisasa lenye maduka yenye aina mbalimbali za bidhaa ni moja kati ya maduka makubwa yaliyopo jijini Dar es Salaam.
Waokoaji waliokuwepo wamepata wakati mgumu kuzima moto kutokana na ndani ya jengo hilo kuwa na giza nene lililotawaliwa na wingu la moshi uliosababishwa na moto huo.
Wamejitahidi kupata mwanga kwa kuwasha taa za magari karibu na lango kuu la kuingilia ndani lakini ilishindikana.
Mwisho
No comments:
Post a Comment