Mbwana Samatta akifunga bao hilo jana, ambalo lilikuwa la pili kwenye mchezo
NAHODHA wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jana amefunga bao moja timu yake, KRC Genk ikishinda 4-0 Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk dhidi ya Lokeren katika mchezo wa mchujo wa kuwania kucheza UEFA Europa League msimu ujao.
Samatta alifunga bao lake dakika ya 72, likiwa la pili katika mchezo huo baada ya Alejandro Pozuelo kutangulia kuifungia Genk la kwanza dakika ya 45 na ushei, kabla ya Jean-Paul Boetius kufunga la tatu dakika ya 77 na Jose Naranjo kumalizia la nne dakika ya 90.
Bao hilo linamfanya Samatta aliyecheza mechi hiyo akitoka nyumbani kuichezea timu yake ya taifa, Taifa Stars na kuufunga mabao yote katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Botswana Jumamosi iliyopita, afikishe mabao 18 katika mechi 49 alizoichezea Genk tangu asajiliwe Januari mwaka jana akitokea TP Mazembe ya DRC.
Kati ya mechi hizo 49, michezo 18 Samatta alicheza msimu uliopita na 31 msimu huu na kati ya hiyo, ni michezo 30 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na 20 msimu huu.
Mechi 19 kati ya hizo alitokea benchi, nane msimu uliopita na 11 msimu huu, wakati 11 hakumaliza baada ya kutolewa, tano msimu uliopita na sita msimu huu na katika mabao hayo 18, 11 amefunga msimu huu na sita msimu uliopita.
Kikosi cha KRC Genk kilikuwa: Ryan, Castagne, Brabec, Colley, Uronen, Berge, Pozuelo, Malinovskyi/Heynen dk68, Trossard, Boetius/Buffalo dk83 na Samatta/Naranjo dk79.
Lokeren: Verhulst, Maric, Skulason, Person, De Sutter, Galitsios, Ofkir, Hupperts/Stra Sunsetman dk61, Ticinovic/De Prycker dk77, na De Ridder Bolbat/Martin dk58.
No comments:
Post a Comment