Wadau wakifuatilia kwa makini. katika semina hiyo washiriki walifanikiwa kupata cheti, ikiwa ni ishara ya kupata mafunzo hayo |
Na Mwandishi wetu.
Taasisi ya ORATA (Organization Against Transport Accidents) ni kama tumaini jipya kwa sekta ya usafirishaji. Kwa mujibu wa taarifa ambazo mtandao huu umezipata ni kwamba kwa muda mrefu kumekuwa na changamoto nyingi za ajali za barabarani na hakuna tafiti za kitaalamu zilizofanywa zikiwa na lengo la kubaini sababu za kutokea kwake, na kama zimefanyika basi ni chache sana.
Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi,Mkuu wa operesheni kutoka kikosi cha Usalama barabarani Kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Bw. Fortunatus Muslim amesema umoja wa ORATA utasaidia sana kurekebisha baadhi ya changamoto zinazojitokeza katika sekta ya usafirishaji.
Amesema kuanzishwa kwa Taasisi ya ORATA ni habari njema kwa taifa la Tanzania, ambapo anaamini kwa majukumu yao mawili ya kufanya tafiti na kuziwasilisha; kutaibua sera mpya ambazo hapo awali zilishindikana kuwepo kutokana na kutokuwepo watu wa kuonyesha sababu za kuwepo.
No comments:
Post a Comment