Wednesday, May 31, 2017

Majabu Kifo cha Ndesamburo,IGP Sirro aanza kwa kasi,Yeriko akamatwa kimafia Dar,Rufaa ya Simba FIFA yaiva,Soma Magazeti ya leo Hapa,Alhamis June 1,2017

Magazetini leo Alhamis June 01, 2017























HIFADHI YA TAIFA MIKUMI MKOANI MOROGORO NI MBUGA ZA WANYAMA AMBAYO HUJIVUNIA IDADI KUBWA YA WAGENI

 Muongozaji wa hifadhi ya taifa milima ya Udzungwa mkoani Morogoro Yustone Bonike akimuonyesha muandishi wa habari wa gazeti la Nipashe Ashiton Baraigwa mbegu ya mimea ambayo inaweza kuliwa na nyani kipindi cha ukosefu wa chakula na kumuletea madhara hatua ya nyani huyo kugeuka kuwa kichaa.
Moja wa maporomoko ya maji kivutio ambacho kina patikana katika hifadhi ya taifa ya milima ya Udzungwa mkoani Morogoro ambacho hufikiwa kilahisi kwa njia miguu na hupatikana ndani ya msitu.
Moja ya myama anayepatikana katika hifadhi hiyo anayejulikana kwa jina maalufu “digidigi” akiwa ndani ya Msitu huo anakula majani.
Hali halisi ya mazingira ya hifadhi ya taifa ya milima yaUdzungwa mkoani morogoro ambapo ofisi zake hupatika humo mbele
Mafundi wakiwa katika ujenzi wa Zahanati katika Kijiji cha Lumango Wilayani kilosa mkoani Morogoro mradi wa ujirani mwema unaotekelezwa na Hifadhi ya taifa mikumi kwa asilimia 70 huku wananchi wakichangia nguvu kazi kwa asilimia 30 nia na madhumuni ya ushirikiano huo ni kulinda na kuhifdhi mipaka ya TANAPA pamoja na kutoa taarifa za ujangili.
Moja ya jengo la Zahanati ambalo limeanza kutumika katika Kijiji cha Ihombo kata ya Mikumi mkoani Morogoro likielezwa kwa mwezi kupokea wagonjwa wasiopungua 300 mradi ambao ulitekelezwa na Hifadhi ya taifa mikumi kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na ujirani mwema dhidi ya ulinzi wa mipaka ya hifadhi hiyo.
Tembo nao ni miongoni mwa wanyama wanaopatikana kwa wingi katika hifadhi ya taifa Mikumi mkoani Morogoro ambao mara nyigi hupenda kutembea kwa makundi na hasa wakati wa kujitafutia malisho kama inayooneka.
Kikundi cha utunzaji wa mazingira kinachotokana na mradi wa utalii wa kitamaduni wakiwa wameshikilia vikapu ambavyo vimetengenezwa na mifuniko ya chupa za maji ambayo wamekuwa wakiyaokota (wapili kutoka kulia ni katibu wa kikundi cha utunzaji wa mazingira Christandusi Mdoe.
Wageni wa kitalii katika hifadhi ya taifa mikumi mkoani Morogoro wakijadiliana kitu nje ya ofisi ya mapokezi huku wakifurahia mazingira ya eneo hilo la wanyama wakionyesha jinsi walivyo na amani katika eneo hilo.
Silas Bakari fundi ujenzi wa nyumba za kitamaduni akionyesha matumizi ya vyumba katika maeneo ambayo yamejengwa na chupa ambazo huokotwa kandokando ya hifadhi ya taifa mikumi na maeneo mengine, jinsi ambavyo chupa hizo zitakavyoboreshwa na kuifanya nyumba kuwa kivutio ch a utalii wa kitamaduni kwa wageni. --- Hifadhi ya Taifa Mikumi mkoani Morogoro ni moja ya mbuga za wanyama ambazo kwa sasa hujivunia idadi kubwa ya wageni na wanyama makundi tofauti wakiwemo simba pia ni hifadhi ambayo hufikika kwa urahisi na kuwafanya wageni kuona wanyama kwa haraka. Hifadhi imeshirikiana na vijiji katika kuunda ujirani mwema kupitia miradi mbalimbali ambayo imekuwa ikiibuliwa na wananchi ili kuhakikisha maafisa wa wanyamapori wanashirikiana na wanavijiji kulinda mipaka ya hifadhi ya taifa mikumi dhidi ya ujangili. Mbuga ya wanyama Mikumi hupokea wageni wa aina mabalimbali wakimiwemo wenyeji wakazi kwa vingilio tofauti ukilinganisha na watalii wandani ambapo vingilio vyao ni shilling 5700 kwa mtu mzima.

STARS KUANZA KUFANYA MAZOEZI USIKU



Timu ya mpira wa miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti kutoka Kampuni ya Bia ya SBL, imesafiri salama kutoka Dar es Salaam, Tanzania hadi hapa Alexandria, Misri.

Timu iliyotumia Ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia, ilipaa kutoka Dar es Salaam, saa 10.45 jioni ambako ilipitia Addis Ababa kuunganisha ndege ya kufika Misri.

Stars iliyokuwa na jumla ya watu 30 wakiwamo viongozi, benchi la ufundi na wachezaji kwa ujumla, ilitua Uwanja wa Ndege ya Cairo, Misri majira ya saa 7.45 usiku ambako mbali ya wenyeji Tolip Sports City, pia ilipokelewa na maofisa wa ubalozi wa Tanzania walioko hapa Misri.

Baada ya kupokelewa, timu hiyo ilisafiri kwa gari maalumu kutoka Cairo, Misri hadi Alexandria umbali wa zaidi ya kilomita 180 na kufika alfajiri baada ya mwendo wa takribani saa mbili. Saa za Misri na Tanzania zina tofauti ya dakika 60. Misri wako nyuma kwa saa hiyo moja.

Kwa niaba ya timu nzima, Kocha Mkuu, Salum Shabani Mayanga pamoja na viongozi wengine akiwamo Mkuu wa Msafara, Wilfred Kidao walishukuru Mungu kwa kusafiri salama hadi kufika hapa Alexandria kwa ajili ya kambi ya wiki moja kujindaa kucheza na Lesotho. Pia walishukuru Watanzania wote kwa dua zao kwa kusafiri salama.

Akizungumza mara baada ya kukagua viwanja vya mazoezi leo asubuhi, Kocha Mayanga ambaye alipewa majukumu ya kuifundisha timu hiyo mapema - Januari, mwaka huu, amesema: “Programu ya mazoezi kwa timu hii itaanza leo saa 2.00 usiku. Ingawa siku nyingine nitafanya asubuhi na jioni.”

Kwa msingi huo, alisema kesho Alhamisi Juni mosi, atakuwa na mazoezi kwa vipindi vyote viwili uwanjani - asubuhi na usiku kabla ya kutoa maelekezo darasani kwa siku ya Ijumaa na baadaye mazoezi ya uwanjani tena.

Taifa Stars inayopiga kambi hapa Misri, inajiandaa na mchezo dhidi ya Lesotho utakaofanyika Juni 10, 2017 kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi nje kidogo ya jiji la  Dar es Salaam. Mchezo huo umepangwa kuanza saa 2.00 usiku.

Mchezo dhidi ya Lesotho ni muhimu kwa Tanzania ikiwa ni mechi ya kwanza kwa Taifa Stars katika Kundi ‘L’ kuwania nafasi muhimu ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika NCHINI Cameroon.

Mbali ya Lesotho na Tanzania, mataifa mengine katika Kundi ‘L’ ni Uganda na Cape Verde ambao pia wikiendi ya Juni 9, 10 na 11, mwaka huu watakuwa katika mchezo wa kwanza pia kuwania nafasi hiyo.

Wachezaji wanaounda kikosi hicho cha Kocha Salum Mayanga ni makipa Aishi Manula  (Azam FC), Benno Kakolanya  (Yanga SC) na Said Mohammed (Mtibwa Sugar).

Walinzi wa pembeni wako Shomari Kapombe    (Azam FC), Hassan Kessy (Yanga SC), Mohammed Hussein (Simba) na Gadiel Michael.

Walinzi wa kati ni Erasto Nyoni  (Azam FC), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba SC) na Nurdin Chona (Tanzania Prisons) ilihali viungo wa kuzuia ni Himid Mao (Azam FC) na Jonas Mkude kutoka Simba SC ambaye kwa sasa anapatiwa matibabu baada ya kupata ajali.

Viungo wa kushambulia Salum Abubakar (Azam FC), Said Ndemla  (Simba SC) na Mzamiru Yassin (Simba) wakati viungo wa pembeni ni Simon Msuva (Yanga SC), Shizza Kichuya (Simba SC) na Farid Mussa (Teneriffe, Hispania).

Washambuliaji wapo Mbwana Samatta (KRC Genk- Ubelgiji), Ulimwengu (AFC Eskilstuna – Sweden), Ibrahim Ajib (Simba SC), Mbaraka Yusufu (Kagera Sugar) na Abdurahman Mussa (Ruvu Shooting).


Wasaidizi wa Mayanga katika benchi la ufundi ni Novatus Fulgence ambaye ni kocha msaidizi Patrick Mwangata - kocha wa makipa pia yumo Meneja wa timu, Danny Msangi; Mtunza Vifaa, Ally Ruvu, Daktari wa timu ni Richard Yomba na Daktari wa viungo ni Gilbert Kigadye.




PICHA: Matajiri Walivyomiminika na Magari ya Bei Mbaya kumzika Ivan wa Zari





MKULIMA MBARONI KWA KUTAPELIWA AKITUMIA SARE ZA JESHI LA WANANCHI TANZANIA -JWTZ

Na Tiganya Vincent, Tabora
Mkulima mmoja Kitangili mkoani Shinyanga Francis Martin Kilalo (31) anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora kufuatia kukutwa na sare na vifaa vingine vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambavyo anatuhumiwa kuvitumia kupateli nakuwadanganya kwa kuchukua fedha kutoka kwa vijana wanaotafuta nafasi yakujiunga na Jeshi hilo.


Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Mkoa wa Tabora, Wilbroad Mtafungwa alipokuwa anaongea na waandishi wa habari ofisi kwake juu ya hatua mbalimbali walizochukua katika kupambana na uhalifu mkoani humo.


Alisema kuwa Polisi walifanikiwakumukamata mtuhumiwa huyo katika Hoteli ya JM iliyopo Wilayani Igunga akiwa na sare mbalimbali za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) zikiwa na cheo cha Koplo ambavyo ni pamoja na kofia tatu, begi, sweta, buti jozi moja, magwanda na mikanda mitatu.


Mali nyingine zilikamatwa kwa mtuhumiwa huyo ni pamoja na fomu za likizo, fomu za kujaza vijana wanaotaka kujiunga na Jeshi hilo na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa mujibu wa Sheria na hiari na mihuli zenye nembo inayofanana na Jeshi hilo.


Kamanda Mtafungwa alisema kuwa mtuhumiwa alikuwa akitumia nyaraka na sare za Jeshi hilo kuchukua fedha kwa kuwadanganya na kuwatapeli wananchi mbalimbali kwa kudai atawatafutia ajira katika majeshi ya Kujenga Taifa na la Wananchi.


Kamanda huyo wa Mkoa wa Tabora aliongeza kuwa mtuhimiwa huyo pia alikutwa na barua kutoka Serikali za mitaa za Dar es salaam na gari aina ya Toyota Starlet yenye namba za Usajili T633 ARF ambalo wanaendelea kuchunguza uhalali wa umiliki wake na ambalo mtuhumiwa alikuwa akilitumia na kuwafanya baadhi ya wananchi wamuamini kuwa atawasaidia kupata nafasi katika majeshi.


Aliongeza kuwa mtuhimiwa huyo na barua za maombi ya watu yakuomba kujiunga na Jeshi, Fomu za Matibabu za Hospitali ya Jeshi ya Lugalo na kalaya Vyeti vya kumaliza elimu ya Sekondari vya baadhi ya watu.


Kufuatia tukio hilo alitoa witokwa waananchi waliowahi kutapeli ndani na nje ya Mkoa wa Tabora kujitokeza katika vituo vya Polisi ili waweze kutoa ushahidi utakasaidia kuonyesha ni jinsi gani walivyumizwa na mtuhumiwa huyo .


Kamanda Mtafungwa alisema kuwa Polisi inaendelea kushirikiana na JWTZ ili iweze kubaini sare na vifaa hivyo alivipata wapi , kwa lengo lipi na ni nani aliyompatia ili wahusika wote waweze kufikishwa katika vyombo vya Sheria kwa hatua zaidi.


Aidha, Kamanda huyo aliwaasa wananchi kuwa makini na matapeli wanaowadai fedha na kuwadanganya kuwa watawatafutia kazi katika Majeshi kwani vyombo hivyo vinaotaratibu wake ambao ndio unaotumika kuwapata vijana wanaojiunga kwa mujibu wa sheria na wale wahiari na sio kwa kuchangishwa fedha.


Wakati huo huo Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora limefanikiwa kukamata watuhimiwa 17 kwa kukutwa na lita 205.25 za gongo wakati wa msako wa kukamata wa watumiaji na wauzaji wa bidhaa hizo haramu.


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora Mtafungwa alisema kuwa watuhimiwa watafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zao wakati wowote. Aidha, alisema kuwa katika zoezi hilo pia Polisi ilifanikiwa kuteketeza ekari tano na nusu za mashamba ya zikiwana uzito wa kilogramu 220 yalikuwa yamelimwa katika Msitu wa Hifadhi wa Igombe wilayani Uyui.



Alisema kuwa jitihada za kuwasaka watuhumiwa wa mashamba hayo zinaendelea na kuwaomba wananchi wenye taarifa yawalipo wahusika walisaidie Jeshi la Polisi ili wahusika waweze kufikishwa Mahakama kujibu tuhuma zao.

Kada wa Chadema aeleza Maajabu Kifo cha Ndesamburo,Afa akisaini Rambirambi ya Lucky vicent

Mzee Philemon Ndesamburo Kiwelu, Mbunge mtaafu wa Moshi mjini amefariki dunia muda mfupi uliopita katika hospitali ya KCMC alikokimbizwa kwa matibabu baada ya kujisikia vibaya akiwa nyumbani kwake Moshi.

Jana alimpigia simu Mayor wa Arusha Kalisti Lazaro kwamba aende Moshi akampatie mchango wa rambirambi kwa wanafunzi wa Lucky Vincent. Leo asubuhi Mayor Kalist na kamanda Bahati David wakasafiri kwenda Moshi kupokea mchango huo. Wakati mzee Ndesamburo anaandika cheque akaishiwa nguvu. Wakamkimbiza KCMC ambapo mauti imemfika huko.

Nimepokea kwa mshtuko taarifa za kifo cha Baba yetu huyu. Mwanzoni mwa mwezi huu tulimtembelea nyumbani kwake, mimi na Kamanda Imma Saro. Tulimpigia simu kumsalimia akatualika nyumbani kwake. Tukasafiri kutoka Arusha tukaenda kumuona Moshi. Alikua na afya njema. Tulizungumza mengi, akitushauri na kutufundisha mambo mbalimbali kuhusu siasa. Sasa ndio nagundua kwamba aliikua akitupa wosia.

Pumzika kwa amani baba. Umepigana vita njema, kazi umeimaliza. Tutaonana Paradiso.!

Malisa GJ

R.I.P NDESAMBURO


Mbunge wa zamani wa Moshi Mjini (Chadema) Philemon Ndesamburo amefariki dunia ghafla leo, wakati akipata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC, Moshi.

ORODHA NA DONDOO ZINGINE ZA KOCHA PHIRI TANGU ALIPOJIUNGA NA MBEYA CITY FC

YERIKO NYERERE AKAMATWA USIKU

 Taarifa iliyotolewa na Meya wa Ubungo, Boniphace Jacob imeeleza kuwa Nyerere alikamatwa na watu hao ambao waliambatana na Mwenyekiti wa Kijiji cha Mbutu.

“Nimepata taarifa kutoka kwa ndugu wa Yeriko ambao wamenipigia simu alfajiri leo. Wamesema amekamatwa saa tisa usiku na watu hao ambao walivalia kiraia.  Viongozi wa Chadema wanaelekea polisi kufuatilia kwa kina chanzo cha Yeriko kukamatwa,” amesema Jacob

Taarifa zaidi zitakuja