“Tunajivunia kufanya kazi pamoja na chuo cha Biashara cha Harvard kwa kuwapatia wanafunzi uzoefu wa kihalisia wa kufanya kazi katika nchi kama Tanzania” alisema Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu Fredrick Kanga. “Tuna uhakika kupitia ziara hii wanafunzi hawa waliweza kupata ujuzi ambao wasingeweza kupata katika majadiliano ya darasani pekee.”
Mpango huo wa FIELD Global
Immersion ni programu iliyoundwa kuwaimarisha wanafunzi na kuwajengea uwezo wao
wa kumudu na kuweza kufanya kazi kiufanisi katika tamaduni mbalimbali
ulimwenguni. Benki ya Exim ilianza kufanya kazi na wanafunzi hao kwa miezi
kadhaa kabla ya kuwasili nchini. Wakiwa nchini wanafunzi hao walitoa mawazo yao
kwa uongozi, walishiriki katika utafiti na wateja jijini Dar es Salaam na
mwishowe kutoa mapendekezo yao kwa uongozi wa benki. Kusudio la zoezi hili ni
kutoa fursa kwa wanafunzi kupata uzoefu wa kufanya kazi katika mradi wa
uvumbuzi katika mazingira mageni.
Harvard inakiri pia kuwa ziara hii ya kimasomo isingewezekana bila
kuwepo na washirika wa kimataifa.
“Tunaishukuru sana Exim Bank Tanzania na washirika wengine wote wa
FIELD Global Partner kwa yale wanayofanya kwa niaba ya wanafunzi wetu,” alisema
Profesa Juan Alcacer, mkuu wa kitengo cha FIELD. “Wanafunzi wetu wanafaidika
kupita kiasi kupitia ziara hizi na tunategemea kuwa washirika wetu wanafaidika
pia.”
No comments:
Post a Comment