Friday, May 26, 2017

IRENE UWOYA KUWA BALOZI WA KAMPUNI YA SIMU ZA MKONONI ZA ITEL TANZANIA

Akimtambulisha mapema leo jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Hyatt regency - kilimanjaro, Afisa habari wa kampuni hiyo Bw.Wolle Ferdinand amesema wameamua kufanya hivyo kwa kuwa msanii huyo wa filamu Tanzania amekuwa akielimisha jamii kupitia kazi yake ya sanaa hivyo anaamini ataweza kuzitangaza bidhaa zao na kuunganisha Itel Mobile na watanzania kwa ujumla.

"Sisi Itel Mobile Tanzania tumefanya makubaliano ya kushirikiana na Irene Uwoya kwa muda wa mwaka mmoja kuanzia sasa, Tunaamini kupitia yeye ataweza kuunganisha Itel Mobile na watanzania kwa ujumla wao"alisema.

Msanii wa bongo movie Irene uwoya akisaini mkataba kuwa balozi wa kampuni ya Itel Tanzania mapema leo jijini Dar es salaam


Nae msanii huyo wa filamu ameeleza jinsi alivyofurahi kufanya kazi na kampuni ya Itel Mobile Tanzania huku akiahidi kuwa balozi bora wa bidhaa zao na kufanya kazi kwa moyo wote ili kuhakikisha kilichokusudiwa na kampuni hiyo kinatimia kwa kufikisha ujumbe kwa watanzania.

"Ninaamini Itel mobile Tanzania hawatajuta kufanya kazi na mimi kwani sitawaangusha na naahidi kuwa balozi bora kwa kipindi hiki chote cha mkataba wetu."alisema

msanii wa bongo movie Irene Uwoya akibadilishana nyaraka na Mkurugenzi wa Itel TZ Cooper Chan baada ya kusaini makubaliano ya kuwa balozi wa kampuni hiyo.


Aidha Mkurugenzi wa Itel Mobile Tanzania Bw.Cooper Chen amesema tukio hilo linaleta tafsiri kamili ya mafanikio ya kampuni  kwani mpaka sasa ina umri wa miaka 10 tangu kuanzishwa kwake na imekuwa ikitamba kwa kusambaza bidhaa zake kwenye zaidi ya nchi 45 duniani kote huku ikishika nafasi ya kwanza kati ya  kampuni tatu bora za simu kwa mwaka 2016 ikiwa imeuza zaidi ya simu millioni 50 barani Afrika.

Irene Uwoya akiongea na waandishi wa habari baada ya kuhidhinishwa kuwa balozi wa Itel Tz

Pia,Afisa masoko wa kampuni hiyo Bi.Asha Mzimbili amewaeleza wanahabari kuwa wanazalisha bidhaa bora za mawasiliano na zenye kuridhisha kwa wateja wao  wakiamini ni sawa na kuisaidia jamii katika kuleta maendeleo kupitia muunganiko kati ya jamii za ndani na kimataifa kwa ujumla.

Sambamba na hilo kampuni ya Itel imezindua simu yao mpya ya Itel S31 yenye sifa nyingi ikiwemo ya upigaji picha nzuri kwa kutumia kamera ya mbele(Selfie) katika eneo lenye mwanga afifu pia inaweza kukaa na chaji kwa muda mrefu tofauti na simu zingine zilizowahi kutengenezwa.

Mkurugenzi wa kampuni ya Itel tanzania Bw Cooper Chan akiongea na waandishi wa habari kwanini waliamua kumpa Irene Uwoya ubalozi wa Itel Tz.

Balozi mpya wa Itel tz irene uwoya akipiga picha ya pamoja na wafanya kazi wa Itel TZ.

No comments: