Serikali kupitia Mamlaka ya udhibiti wa mbolea Tanzania (TFRA) imeanzisha
mfumo wa uwagizaji wa mbolea kwa pamoja(BULK PROCURENT SYSTEM) baada ya
kujiridhisha kupitia kikosi kazi kilichoundwa na wizara ya kilimo,mifugo na
uvuvi ambacho kilifanya upembuzi na kukusanya maoni ya wadau kupitia vikao
mbali mbali na kupata maoni toka kwa taasisi za serikali ambazo zimekuwa
zikisimamia mfumo wa ununuzi wa petrol kwa pamoja kama EWURA,PBPA na FCC ili
kupata uzoefu kuhusu mfumo huo.
Akitolea ufafanuzi huo leo katika ukumbi wa idara ya habari maelezo Jijini
Dar es salaam,Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya udhibiti wa mbolea Bw.Lazaro
Kitandu amesema serikali kupitia Mamlaka hio imeanzisha mfumo huo ili
kuimarisha utaratibu wa usambzaji wa mbolea ambapo wadau wote watapata uhakika
wa upatikanaji wa mbolea kwa bei ya ushindani,pia itawawezesha wafanyabiashara
wadogo kukua na kushiriki katika biashara ya mbolea.
Aidha ,Bw.Kitandu amesema kuwa wizara ya kilimo ilisha andaa kanuni za
kusimamia ununuzi wa mbolea kwa pamoja
yaani Fertilizer (Bulk procurement)Regulation G/N NO.49/2017 ambayo
ililindiwa na waziri mwenye dhamana kwa mujibu wa sheria ya mbolea Namba 9 ya
mwaka 2009 kifungu cha 51 na kanuni zake za mwaka 2001,kuwa itatangazwa zabuni
kwa ushindani(compitative bidding)na mfumo upo wazi kwa mtu yoyote kushiriki
kwa kuzingatia taratibu za kanuni hizo.
Waandishi wa habari walioudhuria mkutano huo uliofanyika idara ya Habari maelezo mapema leo jijini Dar es salaam |
"Kanuni za ununuzi wa mbolea kwa pamoja zinaelekeza kwamba uagizaji wa
mbolea kutoka nje ya nchi lazima ufanyike kupitia utaratibu ulioainishwa ambao
ni kwa kutangaza zabuni kwa ushindani(compitative bidding) na kwamba mfumo upo
wazi kwa mtu yoyote kushiriki."alisema
Hata hivyo, mbolea ni moja ya kichocheo muhimu katika kuongeza uzalishaji wa
mazao wenye tija na katika nchi kusini mwa jangwa la sahara Tanzania ni nchi
mojawapo yenye matumizi ya chini ya mbolea ya kilo19 za virutubisho kwa hekta
katika ngazi ya wakulima wadogo, kiasi hiki hakiendani na malengo ya azimio la
nchi za SADC kufikia angalau kilo50 kwa hekta moja, na huku mfumo huu ukiwa
utaanza kuagiza mbolea za aina mbili tu kwa msimu wa 2017/2018 yaani mbolea ya
kupandia(DAP)na kukuzia(UREA)na mbolea zingine kufuatia baadae kadri
itakavyoonekana mfumo huu umeleta manufaa kwa mlaji
No comments:
Post a Comment