Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kikosi kazi kinachoshughulikia watu wanaojihusisha na biashara haramu ya usambazaji na utumiaji wa dawa za kulevya kimefanikiwa kuwakamata watuhiwa wanne wa dawa za kulevya katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es salaam.
Kamisha wa Polisi kanda maalum Saimon Sirro akiongena na waandishi wa habari mapema leo ofisini kwake jijini Dar es salaam |
Akizungumza leo na waandishi wa habari, jijini Dar es salaam, Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Simon Sirro amesema watuhumiwa hao walikamatwa baada ya kuwepo kwa taarifa ya kupokelewa kwa mwili wa raia wa Ghana katika hospitali hiyo.
Aidha Kamanda Sirro alitaja majina ya watumiwa hao kuwa ni Omary Wagile (47), Ally Mahamud Nyundo(41) wote ni wafanyabiashara, huku Omary Abdullah Rukola(47), Athuman Amiry Mgonja wote ni wahudumu wa mochuari katika hospitali hiyo.
Sambamba na hilo Bwana Athuman Mgonja katika mahojiano alikiri kuuchana mwili wa marehemu na kuchukua kete 32 za dawa za kulevya ambapo alimkabidhi Omary Wagile mfanyabiashara ambaye aliziuza kwa Ally Nyundo mnyabiashara mkazi wa Tabata jijini Dar es salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiendelea kuchua taarifa toka kwa kamanda Saimon Sirro |
No comments:
Post a Comment