Madaktari wa Brazil wameanza kutumia ngozi ya samaki aina ya Tilapia kutibu majeraha ya moto wakisema ngozi ya aina hiyo ya samaki ina kiwango kikubwa cha madini ya collagen na protein ambayo husaidia majeraha makubwa ya moto kupona haraka.
Wanasayansi hao wameanza rasmi kutumia njia hiyo inayodaiwa kuwa na ufanisi mkubwa zaidi ya kutumia bendeji za kawaida kwa kuwa ngozi ya Samaki hao inasaidia kupambana na maambukizi ya bakteria wanaoshambulia majeraha ya moto ikiwa na madini yanayosaidia kufuta alama za kuungua kwa haraka.
Inaelezwa mpaka sasa zaidi ya wagonjwa 56 waliotibiwa kwa kutumia ngozi ya Samaki hao wameonesha maendeleo mazuri. Kwa mujibu wa madaktari hao ngozi ya Nguruwe pia inaweza kutumika kufungia vidonda vinavyotokana na moto kutokana na kiwango kikubwa cha collage iliyopo kwenye ngozi hiyo.
No comments:
Post a Comment