BALOZI WA Umoja wa Ulaya nchini mhe. Van De Geer Roeland amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome na timu yake. Mazungumzo hayo yamefanyika ofisini kwa Katibu Mkuu Prof Mchome mjini Dodoma. Katika kikao hicho suala la upatikanaji wa haki kwa watu wote nchini hususan watu wasio na uwezo lilijadiliwa ikiwa ni pamoja na kuimarisha na kuboresha mahusiano mazuri baina ya Wizara na Umoja wa Ulaya. |
No comments:
Post a Comment