Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC) kimeibuka na
kupinga vikali kitendo cha Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA)
kutaka kuiongezea leseni kampuni ya uzalishaji umeme ya Independent Power
Tanzania limited (IPTL) kwa kuwa kampuni hiyo ilishausishwa na kashfa nzito za
uchotwaji mabilioni kupitia akaunti ya ESCROW.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Anna Henga akiongea na waandishi wa habari mapema leo ofisini kwake jijini Dar es salaam, na kushoto ni Ezekiel Masanja Wakili wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu. |
Mnamo juni 7 mwaka huu EWURA ilitoa chapisho kupitia gazeti
la serikali la Daily News kwa kutaka maoni ya wadau kuhusu kuiongezea mkataba
kampuni hiyo wakati mkataba kati ya serikali na IPTL ni siri na haitakiwa watu
wengine kujua wala kutoa maoni au mapendekezo.
Kamati ya bunge ya hesabu za selikali (PAC) mwaka 2014
ilitoa mapendekezo mbalimbali kwa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU)
kwa kuweza kuchunguza juu ya umiliki na uwepo wa rushwa kwenye IPTL na wabia wake.
Hivyo basi Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji ilitakiwa
kujiridhisha na mapendekezo ya bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania kupitaia Kamati
ya Hesabu za Selikali na kuacha kukusanya maoni kwa wananchi wasiojua chochote
kuhusu mikataba hiyo.
Waandishi wa Habari wakiendelea kuchukua matukio kwenye mkutano wa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu na waandishi wa habari uliofanyika mapema leo jijini Dar es salaam. |
Aidha kituo cha sheria na haki za binadamu kimetoa
mapendekezo yafuatayo.
EWURA kusitisha mara moja zoezi lake la kukusanya maoni ya
kuiongezea muda kampuni hiyo mpaka serikali itakapotekeleza mapendekezo ya
bunge kupitia kamati yake ya mwaka 2014.
EWURA kujiridhisha uhalali wa kisheria juu ya umiliki, kujiridhisha
pasipo shaka ushirika wa IPTL katika suala zima la akaunti ya ESCROW na tuhuma
za rushwa kwa wamiliki wake.
EWURA kuomba radhi watanzania na wabunge kwa kujaribu
kuirudisha IPTL kwa jamii wakati inafahamu mika 3 nyuma ilikuwa kwenye kashfa iliyozua
mtafaruku ndani na nje ya nchi.
LHRC inapenda kuwakumbusha Watanzania wote, wabunge,
viongozi wadini, vyama vya siasa kuungana kwa pamoja katika kupinga kusudio hili la kutaka kuongezewa mkataba kwa
kampuni ya IPTL.
Serikali kutoa majibu na ufafanuzi wa utekelezwaji wa
maazimio ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu ya kampuni ya IPTL.
Serikali kupitia taasisi zake kuacha kufanya mazingaombwe
kwa wananchi kwa kuwashirikisha katika mambo ambayo hawajui msingi wake na
badala yake wawe wazi katika hatua zote za makubaliano na wawekezaji.
No comments:
Post a Comment