Rais wa TFF, Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Celestine wamepandishwa kizimbani leo jijini Dar es Salaam.
Pamoja na viongozi hao wa TFF, viongozi wawili wakuu wa Simba, Rais Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ nao wamepandishwa kizimbani baada ya wote wanne kushikiliwa na kuhojiwa na Takukuru, jana.
Taarifa za awali zilieleza kuwa Malinzi na Mwesigwa walikuwa wanatuhumiwa kwa matumizi mabaya ya ofisi na utakatishaji.
Lakini jana jioni, Mwanasheria wa Malinzi, Alloyce Komba akasema hakuwa amejua walikamatwa kwa sababu zipi na hakuambiwa.
Mbali na hivyo, Komba alitaka wapewe dhamana kwa kuwa ni wanatu wanaofahamika na wanatakiwa kwenda kwenye usaili wa kuwania uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
No comments:
Post a Comment