Msanii wa hip hop kutoka kundi la Weusi, Joh Makini amedai Watanzania wameacha kushangaa video bali wamejikita kwenye kusikiliza audio zaidi kama ilivyokuwa hapo awali.
Rapper huyo ameiambia E-Newz ya EATV kuwa kitu cha kwanza kwenye muziki ni audio, na kubainisha kuwa kipindi cha nyuma watu walikuwa hawatengenezi video zaidi ya audio kali na zinaishi kwa muda mrefu.
“Baadae ilipoanza mambo ya video ikawa hata mtu akitoa wimbo na video kali wimbo unakuwa mkubwa. Baadae Watanzania walipoacha kushangaa picha, imekuja wakati ukipiga video kali kama wimbo ni wa kawaida hautoki, kwa hiyo cycle ni ile ile, wimbo ni audio kwanza haijalishi video kubwa au ndogo kwa hiyo ngoma kama ni kali kwenye audio inafanya chochote,” amesema Joh Makini.
No comments:
Post a Comment