LICHA ya kuwepo kwa taarifa za kiungo wa Yanga, Simon Msuva kukataa mshahara wa shilingi milioni tisa aliowekewa na Difaa El Jadida ya Morocco, taarifa nyingine zimeibuka zikidai kwamba Waarabu hao wamemuibukia nchini Afrika Kusini ili wamalizane naye, na yeye mwenyewe amesema anasepa.
Msuva ambaye aliibuka mfungaji bora msimu uliopita akifunga mabao 14 sawa na Abdulrahman Mussa wa Ruvu Shooting, kwa sasa yupo Afrika Kusini akiwa na kikosi cha Taifa Stars kinachoshiriki michuano ya Cosafa.
Chanzo chetu makini kimeliambia Championi Jumatano kwamba, pamoja na taarifa zilizovuja kuwa dili lake limeyeyuka baada ya kukataa ofa ya mshahara wa Sh milioni tisa, Waarabu hao hawajakata tamaa kwani wameamua kumpandia ndege hadi Afrika Kusini alipo sasa.
“Yanga ina kila dalili za kupoteza mastaa wengi kipindi hiki, yaani baada ya kusikia taarifa za Niyonzima (Haruna) na Ngoma (Donald) kwenda Simba nilibaki najifariji na Msuva na Chirwa lakini kwa taarifa nilizopata Msuva naye anang’oka maana wale Waarabu wamemfuata hukohuko Sauz wamalizane naye,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kupata habari hizo, Championi Jumatano lilimtafuta Msuva kwa njia ya simu yake ili aweke wazi ishu hiyo, alipopatikana alisema: “Ni kweli dili langu la kwenda nje halijayeyuka kwani timu ile nimeongea nayo na mambo yako safi sema niko bize huku lakini wamenihakikishia kila kitu kuwa sawa, hivyo nina imani nikirudi tu Tanzania nitapaa zangu. “Ninaposema nje simaanishi ni dili jipya ila ni walewale wa mara ya kwanza ndiyo wameendelea kunihitaji kwani hata huku nimezungumza nao, japo nimewaomba wamalizane na waajiri wangu Yanga, kisha meneja wangu ili nikitoka huku niende kwa amani, maana sitaki kuondoka kwa matatizo.
No comments:
Post a Comment