Friday, June 30, 2017

MWALIMU WA SEKONDARI AFUMANIWA AKIFANYA MAPENZI NA MWANAFUNZI WAKE DARASANI


Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe, Mkoani Njombe, Ally Kasinge(pichani) ameagiza kushikiliwa kwa Makamu Mkuu wa shule ya sekondari Wanike, iliyopo katika wilaya hiyo baada ya kukamatwa akifanya mapenzi na mwanafunzi wake darasani usiku.

Kasinge ametoa agizo hilo baada ya kuwepo taarifa ya kuwepo kwa watu wanaotaka kumsaidia mwalimu huyo kuvuruga ushahidi kwa kupanga na wanafunzi wenye ushahidi huo kuongea tofauti na tukio.

"Kuanzia wanafunzi waliotimuliwa wahojiwe na polisi na wale wanafunzi wengine waliotajwa pia wahojiwe na polisi na mwalimu mwenyewe pia aendelee kushikiliwa .Huyo ambaye anatuhumiwa aendelee kushiliwa na polisi mpaka tupate majibu, kwa sababu akibaki nje ataendelea kutengeneza mazingira ya kutengeneza mtandao wa kutaka kumsaidia na kupotosha ushaidi" alisema Mkuu wa Wilaya Ally Kasinge

Mbali na hilo shule ya sekondari ya Wanging'ombe pamoja na Wanike zimepandishwa hadhi na sasa zitapokea wanafunzi wa kidato cha tano, walimu wa shule hizo wameweka wazi kuwa shule hizo zinachangamoto ya walimu wa sayansi ambao ni wachache ukilinganisha na walimu wa masomo ya sanaa.

No comments: