Taasisi inayotoa
huduma na ushauri wa kisheria na masuala ya haki za watoto na vijana ya Lecri Consult.
Leo tarehe 30 ya mwezi juni imewakutanisha vijana zaidi ya 100 waliomaliza vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini lengo
likiwa ni kuwajengea uwezo wa kujitambua na kutambua fursa zilizopo mbele yao.
Mkurugenzi Mtendaji ambaye pia ni Mwanasheria wa Lecri Consult Bi. Edna Kamelek akiongea na wageni walioudhuria kwenye semina ya uwezeshaji vijana iliyofanyika mapema leo jijini Dar es salaam |
Akifungua semina hiyo mkurugenzi mtendaji wa Lecri Consult Bi. Edna Kamalek alisema kuwa semina hii imelenga kwa vijana waliomaliza vyuo ambao hawana ajira ili kuweza kuwajengea uwezo kutatua changamoto zao na kuwapa ujasiri pindi wanapohitajika kwenye usahili.
“Na kwa wale
vijana waliopenda kujiajiri tunawajengea uwezo wa kujisimamia na kuendesha
biashara zao binafsi” alisema mkurugenzi
Lakini pia
kwa wale vijana ambao tayari wameshapata ajira wanapewa elimu, miiko na maadili
ya kazi ili kuweza kuboresha ufanisi wao na wasifanye kazi kwa mazoea.
Naibu Mkurugenzi ofisi ya Waziri mkuu uamasishaji vijana na uwezeshaji vijana kiuchumi Bi. Esther Riwa kiongea na wageni waalikwa kwenye semina wa uwezeshaji vijana mapema leo jijini Dar es salaam |
Akitoa elimu
hiyo kwa vijana Naibu Mkurugenzi ofisi ya Waziri mkuu uamasishaji vijana na
uwezeshaji vijana kiuchumi Bi. Esther Riwa alisema kuwa tatizo kubwa ni mitaala
tuliyonayo haimjengi mtoto akimaliza aje
kupata ajira. “lakini pia tatizo lingine ni kutofuata maono vijana wengi huchagua
masomo kwa kufuata mkumbo au kwa kushinikizwa na wazazi au walezi wao na mwisho
wake kushindwa kufikia malengo waliyojiwekea ” alisema Bi Esther
Alisisitiza pia
vijana wengi mitazamo yao ni kwamba wakimaliza kusoma moja kwa moja kuajiriwa
na hivyo kushindwa kuzitafuta fursa za kujiajiri kwa kutumia rasilimali
zilizopo hapa nchini kama kama ardhi kuwekeza kwenye kilimo, bahari, mali asili
nk.
Bi. Estha alisema
kuwa vijana wengi wanapenda kuingia
kwenye ujasiliamali lakini hawana mbinu
za kibiashara na matokeo yake ufanya biashara zenye kipato kidogo hali
inayofanya kushindwa kufikia malengo yaliyowekwa na serikali ya kuondokana na
umasikini. Na kwa kupitia semina vijana wataweza kuzinduka na kuziangalia fursa
zenye matokeo mazuri hivyo kupunguza wimbi la umasikini kwa taifa.
baadhi ya wageni waalikwa walioudhuria kwenye semina ya uwezeshaji vijana iliyofanyika mapema leo jijini Dar es salaam |
Bi. Estasia Ngowi akitoa mrejesho baada ya kupata nafasi ya kuhudhuria tena kwenye semina ya uwezeshaji vijana iliyofanyika mapema leo jijini D
ar es salaam
|
No comments:
Post a Comment