Kampuni hodhi ya rasilimali za reli nchini RAHCO ambayo
inasimamia na kutekeleza mradi mkubwa wa ujenzi wa reli ya kisasa ya viwango
vya standard gauge imekwisha mpata mkandarasi atayefanya kazi hiyo,na imekwisha
kabidhi baadhi ya vitendea kazi kwa wataalamu, lakini kulipa malipo ya awali (advance payment) ambayo ni nusu ya
kiwango cha pesa ya mradi wote.
Mkurugenzi mtendaji wa RAHCO,Bw.Masanja Kadogosa ameyasema
hayo alipokuwa ofisini kwake jijini Dar es salaam pindi akiongea na waandishi
wa habari na mkandarasi wa ujenzi ambaye ni ubia kati ya YAPI MERKEZI toka
uturuki na MOTA –ENGENHARIA na CONSTUCAO AFRICA,S.A ya ureno.
Kaimu mkurugenzi mtendaji wa RAHCO Bw. Masanja Kadogosa akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari jana jiji Dar es salaam |
“Serikali kupitia RAHCO imekwisha fanya malipo ya awali (advance
payment) kwa mkandarasi kwa mujibu wa mkataba wa ujenzi ili kazi iweze kuanza
mara moja,lakini tumeshakabidhi jumla ya magari 8 kwa mshauri mwelekezi
anayesimamia mradi .”alisema.
Aidha,mkurugenzi amesema ujenzi huu wa kwanza wa kipande cha
kutoka Dar es salaam-morogoro(km 300)kuna hatua mbali mbali zinaendelea kwa
kuzingatia makubaliano ya aina ya ujenzi wa mradi ambayo ni sanifu-jenga(design
and Build)na muda wa mradi huu kukamilika ni miezi 30 tu,na jumla ya kambi tatu
(3) kwajili ya mkandarasi kufanyia kazi zake zinaendelea kujengwa katika maeneo
ya ilala-shauri moyo(DSM), SOGA (kibaha) na Ngerengere mkoani MOROGORO.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Masanja Kadogosa akikagua ujenzi wa reli ya standrad gauge eneo la ruvu. |
Pia, aliendelea kusema kuwa mradi huu ambao utagharimu dola
za marekani,1,215,282.000 sawa na (Tsh1.2 billion) utausisha sehemu 5 toka Dar
es salaam mpaka mwanza ambapo sehemu zingine zabuni zake zilishatangazwa na
hatua mbali mbali za manunuzi
zinaendelea, ni Morogoro hadi Makutopora (336 km),Makutopola hadi Tabora
(294 km),na maeneo mengine ni Tabora hadi Isaka (133 km),Isaka hadi Mwanza (248
km)huku akiwataka wale wote ambao wapo ndani ya hifadhi ya reli na walikwisha
wekewa alama ya kubomolewa waondoke mara moja kupisha mradi huo.
Hata hivyo,mradi huu ambao ulizinduliwa na mh.Rais wa
Jamhuri ya muungano wa Tanzania JOHN MAGUFULI mnamo tarehe 12/4/2017
unatarajiwa kutoa fursa za ajira kwa wazawa ambapo 20% ya wataalamu watakuwa
watanzania na 80% ya wafanyakazi pia watakuwa ni wazawa.
Wakati huo huo Mkurugenzi wa RAHCO alipata fursa ya kufungua
njia ya daraja la ruvu lililoharibika vibaya kufuatia mvua zilizonyesha kwa
kipindi kirefu hali iliyopelekea kampuni yake na shirika la reli (TRL) kuifunga
njia hiyo mpaka ukarabati ulipokamilika hapo jana.
Ukarabati huo ambao ulifanyika usiku na mchana
majaribio yake yatafanyika kwa kupitisha treni ya mizigo na baadae ya abiria
pindi mainjinia watakapojiridhisha kuwapo kwa hali ya usalama wa njia hiyo
No comments:
Post a Comment