Kiongozi wa Dhehebu la SHIA Ithna Sheria Sheikh Hemed Jalala ameitaka jumuiya umoja wa mataifa (UN) kuiangalia kwa jicho la karibu nchi ya Palestina ili amani iwezekurejea kama ilivyo kwa nchi ya Tanzania.
Kiongozi mkuu wa waislam dhehebu la Shia Ithna ashery Tanzania Sheikh Hemed Jalala akiongea na wageni waalikwa kwenye semina iliyofanyika mapema leo jijini Dar es salaam |
Sheikh Hemed Jalala ameyasema hayo leo katika semina ya Quds ya kuwakumbuka waislamu na wote wanaoishi kwa kupata taabu nchini Palestina, ambapo ameeleza kuwa watanzania inabidi waoneshwe kusikitishwa na kupinga vikali dhidi ya mambo yanayoendelea nchini humo kwani kinamama wanakosa huduma za afya jambo linalopelekea kujifungua kwa taabu.
Sheikh Jalala amefafanua kuwa hali ya nchi hiyo siyo nzuri kwani vijana wa kiislamu wamekuwa wakizuiwa kuswali kwenye msikiti wao mtukufu wa Masjd Aqsa katika swala ya Ijumaa pia wamekuwa wakizuiliwa hata kuswali kwa pamoja (jamaa).
Sheikh Jalala ameendelea na kueleza kuwa imefikia hatua msikiti huo umekuwa unachimbwa mashimo jambo ambalo linaweza kupekea kubomoka kwake.
Baadhi ya wageni walioudhuria semina hiyo ilifanyika Msikiti wa Al Gadar kigogo jijini Dar es salaam. |
Sheikh Jalala amesisitiza kuwa hilo ni jambo la kulaaniwa kwani msikiti huo una maana kubwa kwa waislamu, huku akieleza kuwa ndiyo Qibla chao cha kwanza kwa waislamu (hapo zamani waislamu walipokuwa wanaswali walikuwa wanaelekea uelekeo ulipo msikiti huo), pia ameeleza kuwa kihistoria mtume wao Muhammad (S.A.W) katika safari yake ya Isra na Miraji aliweza kufanya ibada katika eneo hilo takatifu hivyo ni eneo adhimu kwa umma wa kiislamu.
Sheikh Jalala ameitaja hali ya hatari ya msikiti huo na kueleza kuwa haumilikiwa na waislamu kwa asilimia miamoja pamoja na mali zake, hivyo umoja wa mataifa ni vyema ikafanyika juhudi kuirejesha haki hiyo kwa waislamu kwa amani.
Sheikh Hemed Jalala ameongeza kuwa siku ya Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani itakuwa ni siku maalum ya kuwakumbuka wanyonge wa Palestina na kufikisha ujumbe kwa dunia kuwa wanahitaji kusaidiwa, ambapo kutakuwa na maandamano maalum yatakayo anzia maeneo ya Ilala Boma wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Wasomaji wa Quran toka nchini Irani wakisherehesha tafrija hiyo mapema leo jijini Dar es salaam |
No comments:
Post a Comment