Watanzania
wametakiwa kuepuka na kuachana na matumizi ya Zebaki(Mercury) kwenye maisha yao
ya kila siku kwani madini hayo ni hatari kwa vizazi vya sasa na baadae. Hayo yamezungumzwa
mapema leo kwenye semina iliyofanyika ofisi za Mtandao wa jinsia Tanzania(TGNP)
ikiwa na wawezeshaji toka Agenda for Inviroment and Responsible Development.
Afisa program Mkuu wa Agenda Mr. Silvani Mng'anya akitoa ufafanuzi juu jambo mapema leo jijini Dar es salaam. |
Akitoa mawasilisho hayo kwa wanaharakati na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es
salaam afisa mkuu wa programu agenda Mr Silvani Mnganya alisema kuwa watanzania
inabidi tuachane na matumizi ya zebaki na kuangalia mbadara wake katika kila
sehemu ambayo ilikuwa ikitumika kwa faida zetu na jamii kwa ujumla.
Alisema watu
wengi tunatumia au tunawekewa bila wenyewe kujua madhara yake kwa baadae. Zebaki
ni dawa na hutumika kuzibia meno yaliyotoboka ambayo kitaalamu huitwa (Dental Amalgam).
lakini pia
hutumiwa na wachimbaji wa dhahabu na makaa ya mawe kwa kichoma na inapochomwa
moshi wake ni hatari kwani yenyewe inasambaa kwa njia ya hewa hivyo huathiri
viumbe vyote vinavyovuta hewa hiyo.
Vipodozi wanavyotumia
wanawake kuchubua Ngozi vingi huwa vina madini ya Zebaki mfano sabuni ya Jaribu
na Ricco ambazo zilikatazwa na serikali kwani ni hatari kwa ngozi zao na pia
kusababisha magonjwa kama kansa na mengineyo.
Baadhi ya
vifaa vinavyotumika hospitalini na Mahabara za Mashuleni kama Barometa, vipima
joto na kifaa cha kupimia shinikizo la damu (Sphygmomanometer) vinamadini ya Zekaki
hivyo huathiri watumiaji.
Vingine ni Betri,
Swichi na Taa za umeme, Swichi za Redio na baadhi ya dawa za kuulia wadudu
vimetengenezwa na madini hayo.
Wanaharakati toka sehemu mbalimbali za jiji la Dar es salaam wakifuatilia kwa umakini Semina iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) |
Alisema
zebaki huingia kwenye mazingira kutoka kwenye miamba yenye madini hayo shuguli
za kibinadamu kama Viwanda vinapomwaga kemikali za zebaki ambazo huingaia Baharini,
Mtoni Ziwani na sehemu nyinginezo wananchi wakinywa yale maji au kula viumbe
wanaopatikana mule kama Samaki hupata athari hizo.
Kuchoma Makaa
ya Mawe au takataka za aina nyingi bila kujua ndani kama kuna vitu vimeundwa na
madini hayo hivyo moshi uingia watu na kuwapa madhara.
Lakini pia
kwa wale watu wenye utaratibu wa kuchoma maiti kama Indu na jamii kubwa ya watu
toka Asia kama aliyekufa alizibwa jino au meno basi ule moshi sio mzuri kwa
afya za wananchi wa maeneo ya karibu.
Afisa Program ya Harakati na Ujenzi wa Pamoja TGNP Anna Sangai akiongoza semina iliyofanyika ya makao Makuu ya Mtangao wa Jinsia Tanzania |
Lakini tukiachana
na hayo yote zebaki ina madhara makubwa yafuatayo.
Inasababisha
madhara hasi kwa uzazi kuharibu mbegu za kiume, kusababisha kasoro kwa watoto wanaozaliwa
,kuharibika kwa mimba kwa mtoto wa kike inapunguza maendeleo wakati wa mimba na
katika kipindi cha utoto.
Inaharibu mfumo
wa kuona na kusikia, kutetemeka kwa mwili na kukakamaa kwa misuli, kupooza
ugonjwa wa kukosa usingizi na kuleta udhaifu wa kihisia.
Inasababisha
matatizo ya mishipa ya fahamu hasa hasa kwa wanawake ambao ndio wako katika
umri wa kuzaa.
Inasababisha
uharibifu wa vina saba.
Inasababisha
mzio unaoleta vipele kwenye ngozi, kuchoka na maumivu ya kichwa.
Inapunguza uwezo
wa watoto kufikiri au kuweka kumbukumbu.
Afisa Program wa Agenda bi. Dorah Swai akitoa mawasilisho kwa wanaharakati kuhusu athari za Zebaki kwenye Semina iliyofanyika mapema leo jijini Dar es salaam. |
Hivyo basi
mnamo mwaka 2013 nchi ya japani ikiwa ni mwenyeji iliungana na nchi nyingine 56
kuweza kuunda mkataba wa MINAMATA ambao ulikuwa na lengo la kupunguza
ikiwezekana kuondoa kabisa matumizi ya Zebaki katika nchi wanachama. Na kwa
sasa nchi hizo zimefikia 128 Tanzania ikiwemo katika nchi wanachama kwa kuwa ilionekana
nchi zinazoendelea ndizo zinatumia sana madini haya katika shughuli zake.
Afisa program Bw. Fikiri Rajabu akitoa mawasilisho yake kwenye Semina ya kupinga uwepo wa Zebaki kwa matumizi yetu ya kila siku iliyofanyika makao makuu ya TGNP jijini Dar es salaam |
Dada Veronica Magayane akichangia mada kwenye Semina iliyofanyika Makao makuu ya Mtandao wa Jinsia Tanzania Mabibo jijini Dar es salaam |
Dada Janeth Mawinza akichangia maada kwenye Semina iliyofanyika mapema leo jijini Dar es salaam |
No comments:
Post a Comment