Leo ikiwa ni tarehe 2 ya mwezi wa 6 mtandao wa jinsia nchini
TGNP umeandaa ziara fupi kwa madiwani wa kata mbalimbali za jiji la Dar es
salaam lengo likiwa ni kuwapa elimu ya ujasiriamali na utawala bora. ziara hiyo
ilianzia makao makuu ya mtandao huo yaliyopo mabibo jijini Dar es salaam na
kwenda mpaka Kipunguni huko waliweza kupokelewa na mwenyeji wao ambeye ni
diwani wa kata hiyo Bw. Mohamed R. Msophe.
Katika ziara hiyo waheshimiwa madiwani waliweza kujifunza
mambo mbalimbali yahusuyo kilimo kama kilimo rahisi cha mboga mboga ambacho
hakichukui nafasi kubwa na mboga hizo zinapandwa kwenye viroba vyenye mchanga
mfano wa maua. Lakini pia waliweza kuona kilimo cha pili pili miwa pamoja na
mahindi .
|
Baadhi ya madiwani wakipewa elimu na mwenyekiti wa sauti ya jamii kipunguni bw.Selemani Bishagazi juu ya upandaji wa mbogamboga kwa kutumia viroba, mifuko ya kawaida na plastiki za maji |
Akiongea na waandishi wa habari pamoja na madiwani hao Mh. Mohamed
Msophe ambaye ni Diwani wa kata hiyo alisema kuwa kata ya kipunguni imekuwa na
maendeleo kutokana na ushirikiano uliopo kati ya viongozi na wananchi. Na wananchi
wameweza kufichua maovu mengi kama kuna baadhi ya watu walikuwa wakiendeleza
shughuli za ukeketaji, na pia kuweza kutoa ripoti ya gesti bubu na hatimaye aliweza
kuzifunga kutokana zimesababisha mimba kwa watoto wengi na baadhi ya maovu
mengine yaliyokuwa yakiendelea katika kata hiyo.
|
Madiwani walipotembela kituo cha Taarifa na maarifa waliendelea kupewa elimu na Bw. Selemani Bishagazi hususani ufanyaji kazi wa kituo hicho. |
Lakini pia waliweza kuunda vikundi mbalimbali vya wakina
mama, vijana pamoja na wananchi wote kwa ujumla lengo likiwa ni kuweza
kusaidiana wote kwa kuweka fedha na baadae wanachama kuja kukopa. Hii ilisaidia
kumpa nguvu diwani kwenda kuwaomba wadau mbalimbali wa sharia kuja kuwasaidia
kujua haki zao na mambo mengine yanayowazunguka. Lakini pia kubwa zaidi aliweza
kumtafuta mfadhili kwa ajili ya kilimo na ufugaji wa samaki kwa nguvu
walionyesha mfadhili aliaidi kutoa fedha kwa mradi huo.
|
Katibu wa wakulima wa mbogamboga kata ya Kipunguni mtaa wa Amani Bi. Tausi S. Msangi akiwaelezea Madiwani jinsi walivyoweza kufanikiwa katika kikundi chao kwa kutumia picha. |
Na kingine diwani huyo aliweza kuwaunganisha vijana ambao
walikuwa hawana kazi na wengine walikuwa vibaka kuweza kuwapa fedha kwa ajili
ya kilimo na kwa sasa wameshanunua shamba morogoro na kilimo kinaendelea. Pia vijana wa boda boda na bajaji aliweza kuwatengenezea
umoja ambao umekuwa na faida kubwa na unaweza kuwaingizia faida ya hadi laki na
nusu kwa mwezi kwa michango yao ya shilingi elfu moja kwa kila mwanachama
katika kikundi hicho.
Madiwani hao waliweza kushukuru mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP)kwa
kitu kizuri walichokifanya na walisema wamejifunza mengi sana na kuaidi
kuyafanyia kazi waliyoyapata kwenye semina na mpaka kwenye ziara hiyo. Na pia
wametoa ahadi ya kuleta mrejesho endapo wataitwa tena mwakani ili kuweza
kuwajuza wanamtandao mafanikio watakayoyapata kutokana semina hiyo.
No comments:
Post a Comment