Wednesday, June 28, 2017

UKWELI KUHUSU NEY WA MITEGO KUZINGUANA NA CHIBU DANGOTE


Kupitia Uheard ya XXL ya Clouds FM leo June 28, 2017 ni story ya Nay wa Mitego ambaye amekuwa akishutumiwa kuachia wimbo mpya Moto siku chache baada ya Diamond Platnumz kuutambulisha wimbo mpya pia Fire kitu ambacho kinadaiwa kuwa ni vita ya chini kwa chini.
Akizungumza kwenye kipindi hiko Nay wa Mitego amefunguka kuhusu hilo akisema sio kweli bali ni story ambazo watu wanazizungumza akidai kuwa muziki wao hauingiliani.
“Hili watu wanaliletea complain na kelele za hapa na pale zitake kutuchonganisha lakini hakuna tatizo lolote. Kwa kifupi ni kwamba mimi na Chibu tuko poa hatuna tatizo lolote. Sasa hivi kila mtu ana mambo mengi. Tumeshakua, tunakutana tukiwa na vitu muhimu tunazungumza.” – Nay wa Mitego

No comments: