Halmashauri
nchini zimetakiwa kutumia vyema fedha zinazotengwa kwa ajili ya kundi la vijana
na wanawake katika kuunga mkono dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ya
kuifanya Tanzania inakuwa nchi ya Uchumi wa Kati na Viwanda.
Hayo
yamebainishwa leo na Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam alipotembelea
Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF) mabapo katika
ziara hiyo aliambatana na Mstahiuki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Bw. Benjamin
Sitta.
“Taasisi
za kifedha zinao wajibu mkubwa katika kufikia adhima hii ya Serikali, lakini
sisi Serikali za mitaa, Halmashauri ziano wajibu mkubwa kuhakikisha zilie
asilimia tano za vijana na tano za wanawake zinakuwa sehemu ya kuchochea
ufanikishaji wa dhamira njema ya Serikali,” alisema Mhe. Mwita.
Aidha
Mhe. Mwita ametoa pongezi kwa uongozi wa Tantrade kutokana na jitihada zao za
kuhakikisha wanasaidia ukuaji wa bidhaa za ndani hasa bidhaa za ngozi ambapo
alisisitiza ni vyema wakaendelea kuweka mkazo katika eneo hilo kabla ya
kuangalia maeneo mengine.
Kwa
upande wake Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Benjamin Sitta amesema kuwa Maonesho
hayo ya Sabababa yamekuwa na manufaa kwa wafanyabiashara wengi na hata kwa
wananchi kuja kujifunza.
Aliongeza
kuwa pamoja na wananchi kuja kujifunza lakini pia imekuwa ni fursa kwa
wafanyabiashara kutengeneza mahusiano na wafanyabiashara wenzao kutoka nchi
nyingine jambo ambalo katika biashara ni muhimu sana.
Nae,
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Edwin
Ratageruka amesema kuwa dhamira yake ni kuhakikisha bidhaa za ndani zinakuwa na
soko la uhakika ndani na nchi ya nchi.
Ameongeza
kuwa kwa kuanzia wamejikita zaidi katika bidhaa za ngozi ikiwa ni njia pia ya
kuwainua wafugaji ambao mazao ya mifugo yao yanatumika katika kutengeneza
bidhaa mbalimbali za ngozi.
“Serikali inatambua umuhimu wa kuthamini
bidhaa za ndani, ndiyo sababu Ofisi ya Waziri Mkuu iliratibu zoezi ambalo jumla
ya vijana 1000 walipatiwa mafunzo ya usindikaji na ushonaji wa ngozi, katika
mafunzo yaliyofanyika Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam tawi la Mwanza,”
alisema Rutageruka.
Rutageruka
ameongeza kuwa katika kuendeleza jitihada hizo Gereza la Karanga (Moshi) na
Kampuni ya Woisso ya Jijini Dar es Salaam zinatarajia kuanzisha viwanda kwa
ajili ya kutengeneza sole ili kuachana na utaratibu wa kuagiza skutoka nje.
Maonesho
ya 41 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam yanafanyika huku azma ya Serikali
ya Awamu ya Tano ikiwa ni kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya uchumi wa kati
na viwanda, kutokana na dhamira hiyo maonesho haya yamepewa kauli mibu isemayo;
“Ukuzaji wa Biashara kwa Maendeleo ya Viwanda.”
No comments:
Post a Comment