Thursday, July 6, 2017

OMMY DIMPOZ ASAINI MKATABA RASMI NA ROCKSTAR 4000 KUWA MANAGEMENT YAKE MPYA


Miongoni mwa habari njema nilizozipokea kutoka kwenye tasnia ya muziki ni pamoja na hii ya staa wa Bongofleva Omary Nyembo a.k.a Ommy Dimpoz kusaini mkataba na Kampuni kubwa ya muziki ya RockStar4000 ambayo pia Alikiba amesainiwa.
Kupitia ukurasa wake wa  Instagram, Ommy Dimpoz alithibitisha hilo kwa kupost video fupi ikionyesha zoezi la kutia saini kwenye mkataba na kampuni hiyo akiwa na Manager wa Alikiba, Seven Mosha na kuandika:>>>”Ni rasmi sasa nimesaini mkataba na kampuni kubwa ya mziki barani Africa #RockStar4000 kama menejmenti yangu mpya.” 

No comments: