Siku chache kabla ya kuanza kwa maandalizi ya msimu ujao wa 2017/2018, kipa wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na Klabu ya Ferroviario de Maputo ya Msumbiji, Mohamed Mwalami ameteuliwa kuwa kocha mpya wa makipa wa klabu ya Simba.
Taarifa kutoka ndani ya Simba zinaeleza kuwa Simba imeamua kumchukua Mtanzania huyo aliyecheza soka nje ya mipaka kwa muda mrefu huku uwepo wa kocha Mkera aliyekuwa katika nafasi hiyo ukiwa haujajulikana.
No comments:
Post a Comment