MWANAMUZIKI maarufu wa nyimbo za asili, Saida Karoli ambaye hivi sasa anatamba na wimbo wake uitwao Orugamba, amefunguka kuwa japokuwa alipitia kipindi kigumu hapo nyuma, lakini aliamini ipo siku Mungu atamuinua tena.
Akizun-gumza na Risasi Vibes, Saida alisema katika hupaswi kukata tamaa hata mara moja, unachotakiwa kufanya ni kujikaza na kuendelea kufanya kile kitu ambacho unakiamini na kukipenda.
“Nyuma nilipata tabu nyingi sana lakini kikubwa ninachokiamini ni kutokata tamaa maishani mwangu maana ningefanya hivyo leo nisingesikika na mtu yeyote tena na Saida ndiyo angeishia hivyohivyo na Chambua kama Karanga lakini niliamini bila kukata tamaa kuwa Mungu ataniinua tena leo hii,” alisema.
No comments:
Post a Comment