Saturday, July 1, 2017

WATEJA WA TIGO KUFURAHIA MAWASILIANO YA BURE KWA MWAKA MZIMA

Kaimu Meneja wa Huduma za Masoko wa Tigo William Mpinga akiongea na waandishi wa habari wakati wa mwendelezo wa uzinduzi 'Jaza Ujazwe Ujaziwe zaidi' Pichani kushoto ni Mkaguzi wa michezo ya kubahatisha Tanzania, Bakari Majjid na kulia Mchekeshaji Lucas Mhavile JOTI.

Meneja wa Mawasiliano Tigo, Woinde Shisael akielezea jambo wakati wa uzinduzi wa J'aza Ujazwe Ujaziwe zaidi' jijini Dar Es Salaam leo


Waandishi wa habari wakichukua matukio wakati wa mkutano huo mapema leo.

Kampuni inayoongoza maisha ya kidigitali, Tigo Tanzania, leo Tarehe 30Juni 2017, imezindua promosheni mpya na ya kusisimua inayoitwa ‘JazaUjazwe Ujaziwe zaidi’ambapo wateja watakuwa wanazawadiwa vifurushi vya muda wamaongezi, data na ujumbe mfupi kila mwezi kwa mwaka moja mzima wanapokuwa wanaongeza salio,iwe ni kwa njia ya vocha za kawaida, e-pin au Tigopesa.
Washindi wa zawadi watapatikana kwa droo ambazo zitachezeshwa kila siku na kila wiki ambapo wateja wote wa Tigo watakuwa na nafasi ya kujishindia GB 30 za data, dakika 3,000 za muda wa maongezi wa kupiga mitandao yote, meseji 3,000 au kujishindia Samsung S8 kwa muda wa mwaka mzima.
Kwa mujibu waTigo, promosheni hii inakuja sokoni kama sehemu ya kampeni inayoendelea ya ‘JazaUjazwe’ ambayo ni shukurani za Tigo kwa wateja wake kwa uaminifu wao usio badilika kwa kampuni hiyo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa  kampeni hizo,Kaimu Meneja wa Huduma za Masoko wa Tigo William Mpinga amesema, “Tigoinathamini mchango mkubwa usio badilika ambao wateja wetu wamekuwa wakitupatia kwa miaka mingi. Hii ndio sababu inayotufanya tuamini kuwa wana haki ya kushukuriwa kwa uaminifu wao. Kama kampuni tunafuraha kwa mara nyingine kuwazawaidia wateja wetu kwa kuwawezesha kuendelea kufurahia dunia yetu  -Huduma zetu zaki pekee”
Mpinga alibainisha kwamba promosheni mpya itaimarisha Tigo kuwa ndio kampuni inayotoa bidhaa na huduma zenye bei nafuu, wakati huohuo itakuwa inaimarisha jukumu lake kama kampuni ya mawasiliano yenye ubunifu zaidi Tanzania.
“Promosheni hii imekuja kufuatia uboreshaji wa miundombinu ya mtandao wetu uliofanyika hivi karibuni ambao unahakikisha utendaji wa hali ya juu wa utoaji wa huduma. Kwetu sisiTigo, kila wakati tunakuwa wabunifu katika kutengeneza mbinu mpya za kusisimua ambazo zinazo imarisha uhusiano wetu na wateja wetu. Promosheni hii ya uaminifu ni njia bora ya kuwazawadia na kuwashukuru wateja wetu kwa kuendelea kutumia huduma na bidhaa zetu.” AlisemaMpinga.
Alithibitisha tena kwamba Tigo imekusudia kuendelea kuwazawadia wateja wake kwa bidhaa na huduma za kusisimua zaidi na akaongeza kwamba“Ubunifu wa huduma na bidhaa zetu unatokanana utafitiwa kina unaolenga kuwaridhisha wateja wetu. Kwa hiyo JazaUjazwe, Ujaziwe zaidi inakuja kukabiliana na mahitaji ya wateja ya  kuwa na hisia ya msisimko kila mara wanapotumia huduma zetu. Tunaamini kwamba wateja wetu watafurahia dakika, SMS au data za ziada wanazo zawadiwa kila mara wanapoongeza salio na hivyo itaboresha mwenendo wa mawasiliano yao” alielezea Mpinga
Mwisho

No comments: