Mkuu wa Idara ya wanawake Wanajeshi wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kikosi 831 KJ Mgulani (Matron wa Kikosi), Kapteni Lamla Balama baada ya kuzungumza na wanahabari Dar es Salaam leo kuhusu shughuli ya usafi waliofanya katika Wodi ya Wazazi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 53 tangu lianzishwe Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),ambayo yatafikia kilele chake kesho nchini.
Askari wa kikosi hicho wakijiandaa kwa kufanya usafi.
Sajini Clever Mnubi, akimkabidhi kifaa cha kuvaa mdomoni kwa ajili ya kuzuia vumbi mmoja wa vijana wa JKT tayari kwa kufanya usafi.
Vijana wa JKT wakijiandaa kwa kufanya usafi.
Hapa wakiwa wamebeba mashuka kutoka wodi ya wazazi tayari kuenda kuyasafisha.
Hapa wakiwa na ndoo za maji.
Usafi wa kuosha mipira ya kulalia ukifanyika.
Kazi ikiendelea.
Mkuu wa Idara ya wanawake Wanajeshi wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kikosi 831 KJ Mgulani (Matron wa Kikosi), Kapteni Lamla Balama (katikati), akielekeza jambo wakati wa kazi hiyo ya kufanya usafi wa mipira ya kulalia.
Dumu la sabuni likifunguliwa.
Usafi wa eneo la kusafishia mipira hiyo ya kulalia ukifanyika.
Shughuli ikiendelea.
Kazi imepamba moto.
Hapa kazi tu.
Vijana wa JKT wakiosha mashuka. Kutoka kushoto ni Martha Mwamfundilo, Judith Didas na Lillian Masawe.
Usafi wa mipira ya kulalia ukifanyika nje ya wodi ya wazazi.
Usafi ukifanyika wodini.
Mkuu wa Idara ya wanawake Wanajeshi wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kikosi 831 KJ Mgulani (Matron wa Kikosi), Kapteni Lamla Balama (kushoto), akishiriki kufanya usafi wodi ya wazazi katika hospitali hiyo. Kulia ni Eunice Kasogoti na katikati ni Clever Mnubi.
Na Dotto Mwaibale
ASKARI Wanawake wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kikosi 831 KJ Mgulani, wamefanya usafi katika wodi ya wazazi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 53 tangu lianzishwe Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),ambayo yatafikia kilele chake kesho nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo , Mkuu wa Idara ya wanawake Wanajeshi katika Kikosi hicho (Matron wa Kikosi), Kapteni Lamla Balama alisema hii ni mara yao ya kwanza kama idara kufanya usafi katika hospitali hiyo.
" Tumeona ni vizuri na sisi kushiriki kazi za kijamii kwa kufanya usafi katika Hospitali hii kwa kushirikiana na vijana wetu 45 na sisi askari wa kudumu 27 ikiwa ni moja ya shughuli ya kuadhimisha siku yetu hiyo muhimu jeshin" alisema Balama.
"Ni kawaida yetu katika kuadhimisha siku ya kuanzishwa jeshi letu sisi kama askari Alisema shughuli kama hiyo imekuwa ikifanyika katika Hospitali zote za Serikali Jijini Dar es Salaam ambazo ni Mwananyamala, Temeke na Amana kulingana na walivyojipanga askari kutoka vikosi tofauti.
Akizungumzia shughuli hizo za usafi na kuchangia damu zinazofanywa na askari hao kuanzia jana na kuendelea leo kwa askari hao kutoka idara ya wanawake kwa kufanya usafi katika wodi ya wazazi, Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Husna Msangi aliwashukuru askari hao kwa kazi hiyo kubwa walioifanya katika hospitali hiyo.
Akielezea jana kuhusu utoaji wa damu waliochangia askari hao alisema utasaidia kwa kiasi kikubwa kukabiliana na changamoto ya damu hospitalini hapo kutokana kuwa na mahitahi makubwa ya damu kwa wagonjwa.
Alisema mahitaji ya damu katika hospitali hiyo ni makubwa hivyo amewaomba wadau wengine wajitokeze kuchangia damu ili kuokoa maisha ya watu ambao wataweza kupoteza maisha kwa kukosa damu.
Mkazi wa Buza Said Khalfan ambaye mke wake alikuwa yupo katika hospitali hiyo kwa ajili ya kujifungua akizungumzia kazi hiyo ya usafi inayofanywa na askari hao aliwapongeza na kueleza inaleta mshikamano baina ya raia na wananchi.
"Ni jambo zuri linalofanywa na askari wetu kwanza kuonekana katika maeneo kama haya wakifanya usafi wakiwa katika mavazi yao ya kijeshi inaondoa woga kwa wananchi waliozoea kuwaona askari hao wakiwa katika makambi yao na kuleta mshikamano" alisema Khalfan.
No comments:
Post a Comment