Thursday, August 31, 2017

SHEIKH JALALA - AKITOA UFAFANUZI WA NAMNA YA KUSHEREKEA EID EL HAJJ

WAKATI  Waumini  wa Dini Kiislam nchini wakiungana na wenzao Duniani kesho  wakiwa wanasherekea sikuku ya Eid  El Hajj,Waumini hao wametakiwa kusherekea sikuku hiyo kwa kuhakikisha wanadumisha amani na upendo katika jamii.

Pia wametakiwa kuhakikisha wanafanya mambo ya kumpendeza mungu katika sikuku hiyo na kuacha kufanya mambo ya kumchukiza Mungu .
Sheikh Mkuu wa Shia Ithnasheria Hemed Jalala akisisitiza jambo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mapema leo jijini Dar es salaam
Wito huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Kiongozi wa Mkuu wa Waislam Shia Ithnasheria Tanzania, Sheikh Hemed Jalala wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia sikuku hiyo, ambapo amesema sikuku hii ni nembo kubwa kwa waislam ,basi hawana budi kuhakikisha wanaijenga jamii isiyokuwa na aina yoyote ya vurugu.

“Nawaomba waislam tutumie sikuku hii katika kujitafakari na kuhakikisha tunailinda amani yetu hapa nchini Tanzania ,kwa kuleta umoja na mshikamano huu kwetu,na tusikubali kufarakana katika jamii”Amesema Sheikh Jalala.
Baadhi ya waandishi wa habari walioudhuria mkutano ulioandaliwa na msikiti wa Al Gadar uliopo Kigogo jijini Dar es salaam

Kiongozi huyo wa kiroho ameenda mbali kwa kuwataka waislam kututumia sikuku hii muhimu kwa kusherekea kwa  kufanya maasi jambo analodai linakwenda kinyume na sheria za dini ya kiislam.
“Mtu anayemkosea Mungu  Siku ya sikuku ya Eid mtu huyu ni kama amemkosea mungu siku ya kiama”amesema Shekh Jalala.

Sheikh Jalala pia ameitaka serikali kuhakikisha wanatumia rasilimali zilizopo hapa katika nchi za  Afrika  zitumike katika kutatua tatizo la ajira.

“Bara la Afrika bado linalinasumbuliwa na matatizo mengi sana ikiwemo umasikini,bado linasumbuliwa na maradhi bado Afrika inasumbuliwa na njaa,basi tunawaomba viongozi wa Afrika kutumia rasilimali zilizopo katika maneno yetu zitumike katika kutatua matatizo ya ajira ili ipatikane jamii yenye kufanya kazi”ameendelea kusema Sheikh Jalala.
 Hata Hivyo,Sheikh Jalala amewataka pia waislam ambao walikwenda kufanya Hija kutumia njia hiyo katika kuhakikisha wanaijenga jamii nzuri isiyo kuwa na aina yoyote ya fujo na mfarakano katika jamii.


No comments: