Thursday, August 3, 2017

BANDA LA MAONYESHO LA MANISPAA YA UBUNGO LAWA LULU MKOANI MOROGORO

Licha ya maonyesho ya kilimo na mifugo banda la Manispaa ya Ubungo limeenda mbali zaidi hasa katika ubunifu wa hali ya juu wa kuonyesha teknolojia ya mashine ya kuvuta maji ijulikanayo kama ’Wind mill/ Water pump ’
Mashine hiyo inauwezo mkubwa sana wa kuvuta maji kutoka mita 150 hata kwenye mito kwenye mabwawa vilevile inaweza ikatoa hata kwenye visima vya ardhini lakini pia inauwezo wa kusafirisha maji kilomita 2.5 hadi kilomita 5 bila kutumia aina yeyote ya mafuta isipokuwa itatumia upepo tu.

Kwa siku mashine hiyo inauwezo wa kunyonya maji kuanzia lita 150,000 hadi lita 400,000 inategemea na mfumo wa upepo na kabla mashine hii haijatengenezwa wataalamu wanatembelea katika eneo husika kuona tabia ya upepo ya mchana na usiku ipoje.

Na baada ya hapo kunauwezekano wa kutengeneza mashine ambayo inauwezo wa kuvuta maji  ya kusaidia familia kuanzia 350 mpaka 3000 wataweza kupata maji vilevile ya kwenye majosho ya mifugo nk.

Jamii inaombwa kuondokana na mawazo mgando kuwa mashine hizo hazifanyi kazi ili kufikia uchumi wa kati kwa kuwa vifaa vyote vya kuunda mtambo huu vinapatikana Tanzania na hii inasaidia kupunguza gharama alisema Laurian A. Mchau mbunifu na mtafiti wa mashine hiyo.

Mtanzania anayetaka kufikia uchumi wa kati lazima awe mbunifu kupunguza gharama ya vitu katika maisha ya kila siku.

Mtambo huu kwa mtu anayeitaji anaouwezo wa kushirikiana na wataalamu kutafuta baadhi ya vitu na kujikuta anakuwa na mtambo huo kwa pesa ndogo tu.
Karibu banda la Manispaa ya Ubungo , Ubungo Mpya , Ubungo ya tofauti!!!

No comments: