Naibu Waziri wa Afya, Maemdeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla (MB),mapema leo Agosti 17,2017 amefanya ziara ya kutembelea vituo mbalimbali vya Afya na kujionea utendaji kazi katika sekta hiyo Mkoani hapa.
Dk.Kigwangalla ametembelea Kituo cha Afya Kaloleni, kituo cha Afya Levolosi, kituo cha Afya Ngarenaro, Kituo cha Afya Daraja Mbili, Kituo cha afya Mkonoo na Kituo cha Afya ambacho kinajengwa cha Muriet Mpya .
Akizungumza wakati wa kutoa maagizo kwenye vituo hivyo amemuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Dk. V.Timothi Wonanji na Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya jiji la Arusha Dk. Baraka Mundhe na viongozi wengine wa mkoa akiwemo kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Rebecca Mongi kuhakikisha wanatatua changamoto za Afya ikiwemo ukosefu wa vyumba vya upasuaji na ukosefu wa vitendanishi katika mashine za vipimo vya maabara.
"Mnavyo vituo vya Afya 7.
Mnahitaji kuwekeza zaidi ili mnunue vifaa vya Maabara na kufanyia ukarabati hivyo vilivyopo. Kuna vifaa vya maabara vya kisasa ambavyo ni ‘portable’ na havina gharana kubwa. Tunataka mtenge fedha za kutosha ili kuimarisha sekta ya Afya" aliagiza Dk Kigwangalla.
Aidha akitoa agizo wakati kukagua kituo cha Afya Daraja Mbili ameagiza mara moja jengo la Chumba cha Upasuaji cha kituo hicho kianze kazi ndani ya wiki mbili na upasuaji ufanyike ikiwemo wataalamu kuwapo hapo muda wote.
"Naagiza ndani ya wiki mbili. Huduma za upasuaji zifanyike hapa kwani mnacho kila kitu , vifaa vingi na vya kutosha na jengo zuri la kisasa" alisema, Dk Kigwangalla.
Katika hatua nyingine Dk.Kigwangalla ameagiza kituo cha Afya Kaloleni kuhakikisha wanajenga wodi ya akina mama na kukamilisha maboresho ya Chumba cha upasuaji.
"Hiki kituo hakina hadhi ya kuwa Kituo cha Afya. Ni sawa na Zahanati tu maana kama hakuna huduma muhimu za upasuaji na wodi ya wazazi, nahitaji kuona munakamilisha mara moja" alieleza Dk. kigwangalla.
Katika hatua nyingine, Dk. Kigwangalla ameweza kukagua sehemu za Maabara, wodi za wazazi na vyumba vya upasuaji pamoja na maeneo mbalimbali ya hospitali kuona utendaji wa kazi muhimu na namna ya utoaji wa huduma zinazotolea katika Jiji la Arusha.
Mbali na kukagua vituo hivyo vya Arusha, Dk. Kigwangalla pia ameweza kutembelea baadhi ya maeneo yanayotarajiwa kujengwa vituo vya Afya kwenye maeneo hayo ya Wilaya ya Arusha.
Naibu Waziri wa Afya, Maemdeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla (MB), akitoa maelezo kwa uongozi wa Kituo cha Afya Kaloleni namna watakavyojenga wodi ya Wazazi katika moja ya maeneo ndani ya kituo hicho cha Afya Kaloleni, Wilaya ya Arusha, mapema leo Agosti 17,2017 wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea vituo mbalimbali vya Afya na kujionea utendaji kazi katika sekta hiyo ya Afya Mkoani hapa.
Naibu Waziri wa Afya, Maemdeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla (MB), akitoa maelezo kwa uongozi wa kituo cha Afya Levolosi juu ya uwekaji wa vifaa vya Maabara hiyo
Dk. Kigwangalla akkagua chumba cha upasuaji katika kituo cha Afya Levolosi
Dk. Kigwangalla akikatisha mitaa kwa miguu akitokea kituo cha Afya Levolosi wakati akielekea kukagua kituo cha Afya cha Ngarenaro
Dk. Kigwangalla akikatisha mitaa kwa miguu akitokea kituo cha Afya Levolosi wakati akielekea kukagua kituo cha Afya cha Ngarenaro
Dk. Kigwangalla akikatisha mitaa kwa miguu akitokea kituo cha Afya Levolosi wakati akielekea kukagua kituo cha Afya cha Ngarenaro. Kulia kwake ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Dk. V. Timothi Wonanji na kushoto ni Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya jiji la Arusha Dk. Baraka Mundhe.
Dk. Kigwangalla akikagua kituo cha Afya ambacho kinajengwa cha Muriet Mpya wakati wa ziara yake hiyo.
Dk. Kigwangalla akikagua kituo cha Afya ambacho kinajengwa cha Muriet Mpya wakati wa ziara yake hiyo.
Dk. Kigwangalla akiwa katika kituo cha Afya Themi wakati wa ziara yake hiyo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Rebecca Mongi
Dk. Kigwangalla akikagua kituo cha Afya kinachojengwa wakati wa ziara yake hiyo.
Dk. Kigwangalla akipata picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa sekta ya Afya Jiji la Arusha wakati wa ziara yake hiyo.
Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya jiji la Arusha Dk. Baraka Mundhe akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla wakati alipotembelea kituo cha Afya Kaloleni.
Dk. Kigwangalla akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) wakati akizungumza na waandishi wa habari
Dk. Kigwangalla akitoa maagizo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Bi. Rebecca Mongi wakati wa ziara yake hiyo ya kukagua vituo vya Afya
No comments:
Post a Comment