Wateja kushinda zawadi murua ikiwemo pikipiki na TV za kisasa kwa kununua simu za Tecno S1 na Tecno R6 kutoka maduka ya Tigo nchi nzima.
Dar es Salaam, Agosti 17, 2017- Kampuni inayoongoza kwa maisha ya kidigitali, Tigo Tanzania imezidi kuwaneemesha wateja wake baada ya kuzindua promosheni kabambe ambayo inawapa wateja nafasi ya kushinda pikipiki na TV za kisasa kwa manunuzi ya simu mpya aina ya Tecno S1 na Tecno R6 kutoka kwa maduka ya Tigo nchi nzima.
Akizungumza katika uzinduzi wa promosheni hiyo murua iliyofanyika katika makao makuu ya Tigo jijini Dar es Salaam, Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael alisema kuwa kupitia promosheni hii Tigo inahakikisha kuwa kila mtu sasa ana nafasi ya kumiliki simu bora ya kisasa kwa bei nafuu. Ikiwa ni muendelezo wa juhudi za Tigo kukuza mabadiliko ya dijitali nchini..
Pamoja na hayo, kwa manunuzi ya simu aina ya Tecno S1 na Tecno R6 kutoka maduka yote ya Tigo nchini, wateja wataingizwa kwenye droo itayowapa nafasi ya kushinda mojawapo ya pikipiki 20 na televisheni 20 za kisasa zinazoshindaniwa katika promosheni hii.
Shisael aliongeza kuwa kila mteja atakaponunua simu aina ya Tecno S1 na Tecno R6 kutoka maduka ya Tigo, wafanyakazi wa Tigo watanakili namba maalum ya utambulisho ya simu (IMEI) pamoja na jina na namba ya simu ya mteja husika aliyenunua simu. Namba hizi zitaingizwa katika droo za kila wiki ambapo kila wiki, wateja watapata nafasi ya kujishindia mojawapo ya pikipiki mbili na TV mbili zitakazoshindaniwa katika droo za wiki.
‘Promosheni hii ya Tecno S1 na Tecno R6 inahusu tu wale wateja watakaonunua simu za aina hii kutoka kwa maduka yetu ya Tigo nchini kote. Simu ya Tecno S1 ni ya mfumo wa 3G na itapatikana kwa bei ya shilingi 99,000/- tu. Simu ya Tecno R6 ni ya mfumo wa 4G na itapatikana kwa bei ya shilingi 195,000/- tu. Simu zote mbili ni za kisasa na zina uwezo wa kutumia mfumo wa data, kwa hiyo wateja wataweza kutumia huduma bora za data za 3G na 4G kutoka Tigo, hii ikiwa inalingana na aina ya simu watakayonunua’ alifafanua.
‘Tigo inawaelewa na kuwathamini wateja wake kwa ushirikiano mkubwa wanaotupatia. Daima tupo mstari wa mbele kuwarudishia shukrani kwa wateja wetu kwa imani kubwa wanayotuonesha siku hadi siku. Kwa hiyo leo tuna furaha kubwa tena kuwapa wateja wetu nafasi ya kumiliki simu hizi mbili za kisasa zinazopatikana katika maduka yote ya Tigo nchini kote. Pia tunawapa nafasi ya kujishindia zawadi hizi kemkem za pikipiki na TV za kisasa zitakazoboresha maisha yao. Tunaamini kuwa hii itawawezesha wateja wetu kuendelea kufurahia huduma zetu bora zinazobadilisha maisha yao ya kidigitali siku hadi siku,’ Shisaeli alimaliza.
No comments:
Post a Comment