Wednesday, August 23, 2017

MAMBO MAKUU MANNE YATAKAYOPATIKANA KWENYE TAMASHA LA JINSIA MWAKA HUU

Shirika lisilo la kiserikali TGNP Mtandao likiwa bado lipo kwenye maandalizi ya Tamasha kubwa la Jinsia linalotarajiwa kufanyika katika viwanja vya shirika hilo vilivyopo Mabibo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Bi. Lilian Liundi akielezea maandalizi ya Tamasha la Jinsia linalotarajiwa kufanyika tarehe 5 mwezi wa 9 makao makuu ya shirika hilo yaliyopo Mabibo Dar es salaam.
Akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari mapema leo makao makuu ya Mtandao wa Jinsia, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo Bi. Lilian Liundi alielezea mambo makubwa yatakayofanyika kwa siku zote nne za tamasha hilo.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa siku ya kwanza watakuwa wakiwapongeza wanawake waliofanya vizuri au kujenga heshima kwenye nchi yetu kama Mama Samia Suruhu kwa kuwa ni mwanamke wa kwanza kuwa Makamu wa Rais nchini kwetu, Mama Prof. Estha Mwaikambo kwa kuwa mwanamke wa kwanza kuwa doctor ndani ya historia ya nchi yetu, Mama Gertrude Mungela kwa kuwa spika wa kwanza wa bunge la Afrika pamoja na Mama Anna Makinda kuwa spika wa kwanza wa bunge mwanamke na wengine wengi waliofanya mambo makubwa kwenye nchi hii.
Baadhi ya waandishi wa habari walioudhuria mkutano wa maandalizi ya Tamasha la Jinsia linaloandaliwa na Mtandao wa Jinsia mapema leo jijini Dar es salaam
Na kwa siku ya pili itakuwa ni siku mahususi kwa ajiri ya kuwawezesha wanawake kiuchumi hapa itaangaliwa mikakati ya serikali na ya kimataifa juu ya ukombozi wa mwanamke na je wanawake wanajua kuwa kuna mikakati iliyowekwa na serikali kwa ajiri yao?..lakini pia kuangalia kuwa fursa wanazozipata wanazitumiaje kwa kuwa kuna mikopo ya mabenki, kuna vikoba na mifuko mingine je inawajenga au inawanyonya wanawake washindwe kufikia malengo endelevu ya miaka mitano?.pamoja na kuangalia changamoto zinazowakuta wanapojaribu kujikwamua kiuchumi ili waweze kwenda sambamba na sera ya viwanda.
Afisa habari wa TGNP Mtandao Monica John akitoa ufafanuzi wa jambo fulani kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mapema ofisi za Mtandao wa Jinsia Mabibo jijini Dar es salaam
Jambo la tatu ni pamoja na uwekezaji katika usawa wa kijinsia na maendeleo endelevu kwa wanawake na vijana hii ina maana ya kuwa katika nchi yetu asilimia zaidi ya 51 ni wanawake na asilimia zaidi ya 60 ni vijana hivyo kwenye maendeleo ni vema kuangali makundi haya kwa kuwa ndio yenye watu wengi zaidi. lakini pia katika uwekezaji sio serikali peke yake hata idara binafsi zinatakiwa kuwapa mafunzo wafanyakazi wake kwa kipindi husika kwani kutokana na teknolojia mambo huwa yanabadirika kila siku. na kingine kuangalia vijana na wanawake wanashiriki kwenye mipango ya kitaifa na kimataifa na je? wanajua faida zake, na pia kuondoa vizuizi kwenye mambo ya maendeleo kwa mfano vijana kuzuiliwa na familia au mwanamke kuzuiliwa na mume kufanya biashara na shughuli nyingine za kujipatia kipato.
baadhi ya waandishi wa habari wakisikiliza kwa umakini kile kinachofundishwa kwenye semina iliyofanyika mapema leo jijini Dar es salaam
Na siku ya mwisho itakuwa ni ujenzi wa nguvu ya pamoja ambapo hapa itakuwa ni majumuisho ya siku zote tatu  na kuangalia wapi harakati hazikufanikiwa ipasavyo kwa ajiri ya kuongeza nguvu kuondokana na huo mkwamo, lakini pia kuchagua vipaumbele na kupaza sauti kwa pamoja ili malengo yaweze kufikiwa na kusiwepo na vikwazo tena vitakavyozuia harakati kusonga mbele.

No comments: