Katika kuisimamia na kulinda haki za binadamu nchini Tanzania
Kituo cha sheria na hakiza binadamu Tanzania LHRC, Leo wameibuka na kukemea
mambo kadhaa yanayoendelea nchini kwa sasa huku wakiitaka serikali kuyafanyia
kazi kwa haraka kwani kuyaacha ni kuendelea kuminya haki za binadamu nchini,
Nchini Tanzania kwa wiki kadhaa sasa kumekuwa kukiripotiwa
mambo kadhaa ikiwemo Bomoa bomoa ya maeneo mbalimbali nchini kupisha shughuli
za maendeeo,kamata kamata ya wanasiasa na kuminywa na democrasia nchini.Baadhi
ya mambo hayo ni pamoja na -------
SAKATA LA TANAPA KUJERUHI WANANCHI
Akizungumza na wanahabari leo Jijini Dar es salaam Kaimu
mkurugenzi wa Kituo hicho Anna Henga ameyataja mambo ambayo wameamua
kuishinikiza serikali kuyaangalia kwa jicho la Tati kuwa ni pamoja na Operation
inayoendeshwa na TANAPA kulinda hifadhi ambapo baadhi ya watu wamekuwa wakijeruhiwa
na askari wa eneo hilo akiwemo kijana mmoja ambaye wamemtaka kwa jina la
Pormoson Losso mwenye umri wa miaka 23 ambaye iliripotiwa kuwa alijeruhiwa kwa
risasi na askari wa TANAPA kwa madai ya kuwa eneo la hifadhi,ambapo LHRC
wamelitaka shirika hilo kuhakikisha kuwa linalinda haki za binadamu wakati
likiendesha mazoezi yake kwani kutokufanya hivyo ni kinyume na sheria za nchi.
BOMOA BOMOA KIMARA
Sakata lingine ambalo LHRC wamelijadili ni kuhusu Bomoa bomoa
inayoendelea ikiendeshwa na TANROADS katika barabara ya morogoro kupisha
upanuzi wa barabara ambapo inasadikika kuwa mpaka sasa wakazi zaidi ya elfu
moja wamebaki bila makazi maalum,huku wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto
ambao wamaweza kupata madhara makubwa kwa hatua hiyo.
Sakata hilo limewafanya LHRC kuitaka serikali na taasisi zake
kuhakikisha kuwa wanazingatia sheria na haki za binadamu wakati wa uendeshwaji
wa zoezi hilo,ili kuepuka madhara zaidi ambayo yanaweza kujitokeza.
WAKUU WA WILAYA NA MADARAKA YAO
Hivi karibuni kumekuwa na taarifa mbalimbali zikiwahusisha
baadhi ya wakuu wa wilaya kutumia nafasi zao kuwaweka ndani baadhi ya wananchi
na viongozi wa kisiasa kwa makosa mbalimbali na wengine wakiwa bila makosa
jambo ambalo limezua mjadala mpana nchini Tanzania.
Sakata ambalo kwa sasa limekuwa likijadiliwa sana ni kuhusu
Mkuu wa wilaya ya chemba Simon Odunga kumcharaza viboko mzazi wa mmoja wa
watoto walioshambulia gari lake na kuvunja vioo kwa mawe,pamoja na lile tukio
la mkuu wa wilaya ya hai Gelasius Byakanwa kuagiza jeshi la polisi kumuweka
ndani mwalimu Erasto Mhagama wa shule ya secondary lerai kwa kosa aliloliita
utovu wa nidhamu la kushinda kutaja jina la mkuu huyo wa wilaya na kushindwa kutaja
nafasi ya ufaulu wa shule hiyo kitaifa kwa mwaka 2015.
Kwa kuzingatia matukio hayo LHRC wameitaka wizara ya nchi
ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa kuwaonya wakuu hao wa wilaya
kwani matukio hayo yamekuwa yakiongezeka na hakuna sheria inayowaruhusu kufanya
hivyo nchini.
Kufwatia matukio kadhaa ya polisi kuwaua Raia ambao wamekuwa
wakiripotiwa kama wahalifu LHRC imeitaka serikali kuwapa mafunzo polisi ya
kuwaweka kizuizini wahalifu badala ya kuwaua kwa kuwa hakuna shEria inayoruhusu
kufanya hivyo na uwezo wa kuwakamata wanao.
MIILI INAYOOKOTWA UFUKWENI
Kutokana na kuwepo kwa Taharuki kubwa miongoni mwa Taifa
baada ya kuripotiwa kuokotwa ka miili ya binadamu kadhaa inayoelea katika mito
na bahari ya hindi bila kujulikana ni watu gani na ni nani anayewaua huku miili
hiyo ikiwa imefungwa katika viroba,kituo hicho kimeitaka Ofisi ya upelelezi wa
makosa ya jinai DPP kufanya uchunguzi wa miili na matukio hayo ili kutoa
taarifa sahihi ambayo itawatoa hofu wananchi,kwa kuwa vitendo vya mauaji ya
kinyama kwa binadamu kama hayo ni uvunjifu mkubwa wa sheria na haki za binadamu
na watanzania wana haki ya kufahamu matukio hayo yanafanywa na watu gani ili
kurudisha amani mingoni mwa watanzania.
KAMATA KAMATA YA WANASIASA
Kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC kimeelezwa
kusikitishwa kwake na vitendo vya kuminywa kwa democrasia nchini na haki za
kisiasa na kiraia, ambapo hali hii imejitokeza kwa kuwanyanyasa wabunge na
viongozi hasa wa vyama vya upinzani, ikiwa ni pamoja na kamata kamata ya
viongozi hao inayoendelea bila kufwata sheria za nchi,misingi na haki za
binadamu.
Akitolea mfano sakata la kukamatwa mara kwa mara kwa Mbunge
wa singida mashariki Mh Tundu Lissu,ambapo kwa sasa amekamatwa Tarehe 22 mwezi
huu akiwa mahakama ya hakimu mkazi kisutu kwa shughuli zake kwa tuhuma za uchochezi
na baadae kupekuliwa nyumbani kwake.
Wabunge wengine walokumbwa na kadhia hiyo ni Ester Bulaya
mbunge wa Bunda,Godbles Lema mbunge wa Arusha mjini ambaye alikamatwa kwa kosa
la kuzidisha muda wa mkutano kwa dakika saba na maadae kuachiwa.
LHRC wameitaka serikali kutoa nafasi kwa vyama vyote kufanya
kazi kwa usawa bila kuingiliwa kwani Tanzania ipo katika mfumo wa vyama vingi na
ni haki ya kikatiba kwa wanasiasa kuendesha shughuli zao.
No comments:
Post a Comment