Thursday, August 10, 2017

PICHA - BILLGETS AMEKUJA KUJIFUNZA CHANJO YA MATENDE NA MABUSHA BONGO

BILIONEA namba moja duniani na Mwanzilishi wa Kampuni ya Microsoft, William Henry Gates III, ‘Bill Gates’ametua nchini kwa ajili ya kujifunza namna ya utoaji chanjo kwa magonjwa ya Matende, Mabusha, Minyoo na mengineyo katika Wilaya ya Muheza mkoani Tanga.


Gates alifika jana katika Kijiji cha Kicheba na kujifunza namna gani chanjo ya magonjwa ya Matende, Minyoo, Mabusha na mengine ya aina hiyo inavyotolewa, kisha akapata chakula na watoto yatima Kata ya Kicheba, kabla ya saa 7 mchana kurudi tena Tanga mjini.

Hata hivyo, ujio wake ulikuwa wa kimyakimya bila kuwa na mbwembwe nyingi kama ambavyo watu wengi wamezoea kuwaona watu maarufu wa aina hiyo wakifanya ingawa inasemekana anahitaji kuonana na Rais John Magufuli.

Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Hajat, Injinia Mwanasha Tumbo amethibitisha ujio wa bilionea huyo kutembelea wilayani kwake.

“Amekwishaondoka, ugeni wake ulikuwa ni wa saa chache tu kwa ajili ya kujifunza namna ya chanjo ya magonjwa mbalimbali inavyotolewa, baada ya hapo akarudi Tanga.

No comments: